January 10, 2013

MATALUMA KUFUNGUA MWAKA NA VIBAO VIPYA


Na Elizabeth John
MSANII wa muziki wa Bongo Fleva nchini, Juma Mataluma ‘Mataluma’ amesema kuwa kwa mwaka huu amejipanga kuachia ngoma mfululizo kama wanavyofanya wasanii wengine wakiwemo chipikizi.

Akizungumza jijini  Dar es Salaam Mataluma alisema kuwa kwa mwaka jana hakuwa na kubwa alilolifanya na mwaka huu ni wake wa kuonesha kuwa yuko vizuri katika muziki wa kizazi kipya na hajapotea kwenye ‘game’.

“Sijapotea kwenye game kwani kipindi chote nilichokuwa kimya nilikuwa natoa nafasi kwa wengine kuachia zao wakati nikiwa najipanga kufanya vitu vikubwa ili kuhakikisha narudi vizuri kwenye tasnia ya muziki huu ambao umejaa ushindani mkubwa,” alisema Mataluma.

Msanii alisema kuwa kwa sasa yuko mbioni kuachia wimbo unaoitwa ‘Bado Sijafulia’ kwa lengo la kuwajibu wale wanaodhani kuwa ameshiwa na amepotea katika tasnia ya muziki wa kizazi kipya.

Msanii huyo awali alishatamba na nyimbo mbalimbali ikiwemo ‘Kariakoo’ ambao unatoa mafundisho juu ya kutaadhari wizi wa mifukoni unaofanyika eneo hilo na kwenye usafiri wa daladala na wakazi mbalimbali nchini.

Mataluma anawaomba mashabiki na wadau wa tasnia hiyo kukaa vema kupokea kazi hiyo na nyinginezo ambazo zinatarajiwa kuachiwa katika kipindi cha mwaka huu akiwa na lengo la kuwahakikishia wapinzani wake bado yuko vizuri katika tasnia hiyo.

No comments:

Post a Comment

Pages