January 09, 2013

DAVID PRICE KUMVAA TYSON FURY JIJINI LIVERPOOL


David Price akionesha mikanda yake

LONDON, England

BONDIA David Price ameingia makubaliano ya awali kuzichapa na mkali wa masumbwi Tyson Fury katika pambano la uzani wa juu kwa dau nono la pauni milioni 1 hapo Juni mwaka huu, kwenye Uwanja wa Anfield.

Price ilikuwa atetee mikanda yake ya ubingwa wa Uingereza na ule wa Jumuiya ya Madola ‘Commonwealth’ dhidi ya Fury, 24, lakini pambano baina ya wakali hao likaota mbawa.

Promota wa bondia Price, Frank Maloney anajiandaa kukaa kwenye meza ya mazungumzo kwa ya kuboresha ofa ya mpambano huo, ambalo waratibu wakuu wanataka lazima lifanyike mwishoni mwa Juni.

Maloney yu tayari kulipa hata zaidi ya pauni milioni 1, ambapo alisema: “Nimekutana na watu ambao watakuwa tayari kufali mpambano kwa kiasi kizuri zaidi cha fedha.

“Tutahakikisha tunaboresha pambano ambalo hata hivyo hatujaamua litafanyika wapi kati ya Anfield huko Liverpool, au jijini London. Hizo ni sehemu mbili ambazo pambano hili linaweza kupigwa.”

Price, 29, ambaye hajapigwa katika mapambano yake 15 alisema: “Kupigana kwenye dimba la Anfield daima ilikuwa ndoto yangu ya muda mrefu na sasa inaeleka kutaka kutimia hatimaye.”

Bondia huyo amepanda ulingoni mara mbili jijini Liverpool, kumvaa bingwa mara mbili wa dunia Tony Thompson, mabapambano yaliyopigwa kwenye Ukumbi wa Echo Arena.

Price akaongeza kuwa: “Kama sitoongeza idadi ya mapambano hapo, nitakuwa nimetyuma ujumbe muhimu mno duniani kote.”

No comments:

Post a Comment

Pages