January 04, 2013

Dazzy baba kutoka na Sauti zetu


Na Elizabeth John

BAADA ya kuwa kimya kwa muda mrefu, Nyota mkongwe wa muziki wa kizazi kipya nchini, Daud Nyika ‘Dazzy baba’ ameachia kibao chake kipya kinachokwenda kwa jina la ‘Sauti zetu’.

Ndani ya kibao hicho, Dazzy baba amemshirikisha Msanii Mtanzania ambaye anaishi nchini Sweden, anayetikisa katika tasnia hiyo, Man Konka.

Akizungumza jijini Dar es Salaam, Dazzy baba alisema wimbo huo kauachia hivi karibuni na anawaomba Watanzania wausikilize kwa makini kwani ni ujio wake mpya.

“Wimbo huu nimeimba kimaadili, na unavitu vingi tofauti ambavyo mashabiki wangu hawajawahi kuviona kutoka kwangu, hivyo naomba mashabiki wangu waupokee ujio wangu,” alisema Dazzy baba.
Alisema kwasasa yupo katika maandalizi ya kutengeneza video ya wimbo huo, licha kutamba na vibao vingi, ‘Namba nane’ ni wimbo wake ambao ulimtambulisha na kufanya vizuri katika vituo mbalimbali vya redio na runinga.

No comments:

Post a Comment

Pages