January 04, 2013

VIDEO YA NENDA NENDA IKO HEWANI

Na Elizabeth John

HATIMAYE video ya wimbo wa ‘Nenda nenda’ ulioimbwa na mwanadada anayetamba katika tasnia ya muziki wa kizazi kipya nchini, Mwanaisha Nyande ‘Dyna’ imeanza kuonekana katika vituo mbalimbali vya televisheni.

Akizungumza na Habari Mseto jijini Dar es Salaam, Dyna alisema kazi hiyo ameishaizambaza katika vituo mbalimbali na baadhi ya vituo zishaanza kuifanyia kazi.

Alisema anawaomba mashabiki wake waendelee kumpa sapoti katika kazi zake ambazo zinafuata kwani bado kuna burudani nyingi ambazo amewaandalia.

“Kiukweli kazi hiyo haikuwa ya kitoto kwani nimeifanya kwa muda mrefu sana nikiwa na lengo la kuboresha kazi zangu hivyo naamini itakua poa na mashabiki wangu wataipenda,” alisema Dyna.

Dyna ameshawahi kutamba na vibao vingi kikiwemo cha ‘Nivute kwako’ ambacho kilifanya vizuri zaidi kutokana na mashairi ya wimbo huo kusimama na kushirikiana vema na mkali wa muziki huo, Barnaba Elias ‘Barnaba’.

No comments:

Post a Comment

Pages