January 01, 2013

DIMPOZ AWASHUKURU MASHABIKI WAKE


Na Elizabeth John

BAADA ya kutamba na kibao chake cha ‘Me and You’, nyota wa muziki wa kizazi kipya nchini, Omary Faraji ‘Ommy Dimpoz’ amewashukuru mashabiki wake na kuwataka waendelee kumpa sapoti katika kazi nyingine.

Akizungumzia kazi hiyo Dar es Salaam, Dimpoz alisema anawashukuru mashabiki wake kwa kukipokea vizuri kibao hicho ambacho amemshirikisha Mtangazaji wa vipindi mbalimbali vinavyorushwa na kituo cha televisheni cha ITV, Vanessa Mdee. 

Kabla hajatoka na wimbo huo, Dimpoz alishawahi kutamba na vibao vyake kama ‘Baadae’ na ‘Nainai’ ambao ulifanya vizuri na kufanya achukue tuzo katika kinyang’anyiro cha mwanamuziki chipukizi mwaka jana.

“Namshukuru mungu kazi zangu zinapokelewa vizuri na mashabiki wangu, kitu ambacho kinanipa nguvu ya kufanya vitu vizuri zaidi, naomba wapenzi wangu wasichoke kunisapoti,” alisema Dimpoz.

Dimpoz alisema kwasasa anaendelea na maandalizi ya kutengeneza video ya wimbo huo ambao anaimani itafanya vizuri kutokana na mazingira ambayo ameyatumia katika kazi hiyo.

No comments:

Post a Comment

Pages