January 01, 2013

WIMBO WA 2030 WAANZA KUSIKILIZWA REDIONI NA KUONEKANA KATIKA RUNIGA


Na Elizabeth John

WIMBO unaokwenda kwa jina la ‘2030’ ulioimbwa na Msanii Ibrahim Mussa ‘Roma Mkatoliki’ uliokuwa unasubiliwa na mashabiki wa hip hop nchini, umeanza kusikika na kuonekana katika vituo mbalimbali vya redio na runinga.

Wimbo huo umeanza kuonekana na kusikika katika vituo mbalimbali vya redio juzi ambapo Roma amewataka mashabiki wake wakae mkao wa kula kwaajili ya kupokea burudani kutoka kwake.

Akizungumza jijini Dar es Salaam jana, Roma alisema anaomba mashabiki wa Hip hop wakae mkao wa kula kwa kupokea kazi nzuri kutoka kwake baada ya kukaa kimya kwa muda mrefu.

“Naomba mashabiki wangu wakae mkao wa kula kupokea kazi nzuri kutoka kwangu ikiwa ni baada ya kukaa kimya kwa muda mrefu kwa sababu ambazo zipo nje ya uwezo wangu, na sasa nimerudi rami katika ‘game,” alisema Roma Mkatoliki.

Alisema ndani ya kibao hicho kuna mambo mengi amezungumzia ambayo hayapendezi katika jamii, hivyo anawaomba Watanzania wabadilike kwa kupitia wimbo huo.


No comments:

Post a Comment

Pages