January 24, 2013

EDEN HAZARD ALIMPOMCHAPA TEKE 'BALL BOY' WA SWANSEA

VITA nzima ya Eden Hazard na muokota mipira wa Swanzea City - Charlie Morgan, 17, ambaye ni mtoto wa Mkurugenzi wa Swansea, Martin Morgan. Charlie alitembea taratibu kuufuata mpira, Hazard akakimbilia kutaka kuwahisha mchezo, dogo akagombea mpira na nyota huyo, kabla ya kumshuti teke la mbavu kama inavyoonekana pichani.
 Hapa Hazard akimpapatua Charlie ili auchukue mpira tayari kwa kuendelea na pambano. Ikumbukwe hapo Chelsea ilikuwa ikisaka mabao 2-0 iliyofungwa katika mechi ya awali, ili kusawazisha na kulipeleka pambano katika dakika 30 za ziada 'Extra Time' kuwania tiketi ya fainali ya Capital One 'Carling Cup'. Mechi iliisha kwa sare ya 0-0 na Swanse kutinga fainali.
 Alipomshuti dogo Charlie akalala kule akiungulia maumivu na kuuacha rasmi mpira kama unavyoonekana pichani.
 Hazard akauchukua mpira na kurudi nao dimbani akimuacha Charlie akigalala kwa maumivu ya shuti la mbavu. Chezea The Blues wewe dogo!
 Mshambuliaji wa Chelsea Demba Ba ambaye alikiri kumuona Hazard akimpiga teke dogo Charlie, alimfuata dogo kumpa sapoti fulani.
 Charlie katikati akiugulia maumivu baada ya kuinuka.
 Mwamuzi wa mchezo huo Chris Foy, akashindwa kujizuia na kuamua kumlima Hazard kadi nyekundu ya moja kwa moja kama anavyyonekana pichani.
Hapa Hazard akisindikizwa kuingia vyumba vya kuvalia baada ya kuoneshwa kadi nyekundu.

No comments:

Post a Comment

Pages