January 25, 2013

EDEN HAZARD AMUOMBA RADHI ‘BALL-BOY’


Picha tofauti zinazoonesha tukio la Eden Hazard kumpiga muokota mipira 'Ball-boy' wakati wa nusu fainali ya pili ya Kombe la Capital One, kati ya Chelsea na Swansea City iliyoisha kwa sare ya 0-0. Hazard alilimwa kadi nyekundu kwa tukio hilo, ambalo sasa ameomba radhi rasmi.
 
LONDON, England

“Kijana aliukumbatia mpira nami nilikuwa najaribu kuupiga mpira. Na nadhani niliupiga mpira kama nilivyokusudia na sio kijana yule kama ilivyotafsiriwa. Hata hivyo naomba radhi kwa hilo”

NYOTA wa Chelsea, Eden Hazard, amelazimika kukiri kosa na kuomba msamaha, baada ya ‘kujisababishia’ kadi nyekundu ya moja kwa moja kwa kumpiga teke muokota mipira ‘ball-boy’ wakati wa mechi ya Kombe la Capital One dhidi ya Swansea City juzi usiku.

Hazard raia wa Ubelgiji, alionekana akimpiga shuti la mbavu Charlie Morgan, 17, ambaye ni mtoto wa Mkurugenzi wa Swansea Martin Morgan, ambapo baadaye jana alisema hakumpiga kijana huyo.

"Kijana aliukumbatia mpira nami nilikuwa najaribu kuupiga mpira. Na nadhani niliupiga mpira kama nilivyokusudia na sio kijana yule kama ilivyotafsiriwa. Hata hivyo naomba radhi kwa hilo.

"Kijana huyo alikuja katika vyumba vya kuvalia nguo (baada ya mchezo) na tulizungumza mengi ikiwamo kumuomba naye kuniomba radhi na kimsingi tulisameheana vizuri. Limeisha. Naomba radhi," alisema Hazard.

Tukio hilo lilitokea dakika ya 78 ya mchezo huo ulioisha kwa sare ya 0-0, ambapo alionekana kuufuata mpira kwa taratibu, kitu ambacho kilimsukuma Hazard kukimbilia mpira ili kuwahisha mchezo, na kujikuta akigombea mpira huo na kijana huyo.

Mwamuzi wa pambano hilo, Chris Foy alimuonesha mkali huyo kadi nyekundu, na kumtoa mchezoni, kadi inayoweza kumuweka nje ya dimba kwa mechi tatu zilizo chini ya Chama cha Soka (FA).

…..The Sun/BBC……

1 comment:

  1. Vеrу nice artіcle, ϳust what I was lοoking fοг.
    Also see my site :: chalkboards

    ReplyDelete

Pages