January 25, 2013

WATETEZI AZARENKA, DJOKOVIC HAOO FAINALI


MELBOURNE, Australia

Azarenka alilazimika kuyashinda maumivu aliyokuwa nayo kumuwezesha kumng’oa Sloane Stephens na kutinga fainali anakotarajia kupambana na Mchina Li Na

MABINGWA watetezi wa michuano ya wazi ya Australian Open, Victoria Azarenka - Pichani kulia - (wanawake) na Novak Djokovic (wanaume), wamefanikiwa kushinda mechi zao za nusu fainali na kutinga fainali ya michuano hiyo.

Azarenka alilazimika kuyashinda maumivu aliyokuwa nayo kumuwezesha kumng’oa Sloane Stephens na kutinga fainali anakotarajia kupambana na Mchina Li Na.

Azarenka alifanya kazi ya ziada baada ya kupambana huku akikabiliana na maumivu ya enka ya mguu wa kushoto na kushinda 6-1 6-4.

Li Na mkali anayekamata nafasi ya sita ya viwango vya nmchezo huo duniani, alimchapa na kumuondosha Maria Sharapova kwa 6-2 6-2, katika nusu fainali ya kwanza ya michuano hiyo upande wa wanawake.

Kwa upande wa wanaume, Djokovic alimuondoa David Ferrer na kutinga fainali ya michuano hiyo ilinayohitimishwa Jumapili jijini hapa na sasa yu tayari kwa mchuano wa kuwania taji la tatu mfululizo.

Djokovic alitumia muda wa saa moja na dakika 29 kumchapa Mhispania huyo 6-2 6-2 6-1, ambapo anasubiri mbabe wa nusu fainali ya pili wanaume inayochezwa leo Ijumaa kati ya Andy Murray na Roger Federer tayari kwa fainali Jumapili.

…..BBC…..

No comments:

Post a Comment

Pages