January 26, 2013

FERGUSON: HAKI YA MUNGU FA INATAKA KUNITOA KAFARA


MANCHESTER, England

“Nadhani kuna la ziada juu yangu kuliko kile nilichosema. Kama nafikiri kuwa ni haki ama si haki haijalishi katika hali hii ya sasa”


KOCHA wa Manchester United, Sir Alex Ferguson amekoleza moto kauli zake tata, kwa kusema anaamini Chama cha Soka England (FA) kinataka kumtoa kafara.

Ferguson anakabiliwa na uwezekano wa kuadhibiwa na FA, kutokana na tuhuma alizozitoa kwa mshika kibendera wa mechi yao iliyoisha kwa sare ya bao 1-1 dhidi ya Spurs iliyopigwa Jumapili iliyopita.

Mskochi huyo jana alisema: “Nadhani kuna la ziada juu yangu kuliko kile nilichosema. Kama nafikiri kuwa ni haki ama si haki haijalishi katika hali hii ya sasa”

Ferguson alikuwa akihojiwa na FA wiki hii kuhusu tuhuma zake kwa vyombo vya habari dhidi ya mshika kibendera Simon Beck – aliyedai kuinyima timu yake penati halali.

Katika tuhuma zake kwa Beck, Fergie alihoji kiwango cha uchezeshaji kibendera huyo na kusema anadhani alikuwa akiipendelea Spus na ‘kuinyonga’ United.

Na Fergie alisisitiza: “Hicho ndicho nilichokiweka katika barua yangu ya maelezo, lakini nadhani unaijua vema FA. Huwezi kujua. Ni moja tu ya mambo haya. Sisi tuna wasifu wa juu.”

Fergie alikerwa nmakitendo cha Beck, kuichunia aliyoiita ‘penati ya wazi’ iliyotokanana Wayne Rooney kuchezewa rafu na Steven Caulker.

“Mshika kibendera wa upande huu huwa hatoi kitu chochote kwetu kila siku. Kwangu mimi, kilikuwa kiwango kibovu sana cha mwamuzi kumuona akichezesha,” aliropoka Furguson na kuzua mjadala mpana unaoaminika kuwa unaweza kumponza.

…..The Sun…..

No comments:

Post a Comment

Pages