January 04, 2013

HADIJA WA BEST NASSO VIDEONI


Na Elizabeth John
NYOTA wa muziki wa kizazi kipya nchini, Nassoro Hamis ‘Best Nasso’ yupo katika maandalizi ya kuisambaza video ya kazi yake ya ‘Hadija’ ambayo inafanya vizuri katika vituo mbalimbali vya redio.

Akizungumzia kazi hiyo jijini Dar es Salaam jana, Best Nasso alisema alishindwa kuisambaza kazi hiyo kama alivyokuwa maepanga kwaajili ya kupisha sikukuu za Christmas na Mwaka mpya.

“Kesho (leo) ntakuja jijini Dar es Salaam kwaajili ya kuisambaza kazi hiyo ambayo ilitakiwa itoke tangu Desemba niliwaacha wamshabiki wangu washerehekee kwanza afu ndio niwape kitu kipya,” alisema Best Nasso.

Alisema wimbo huo umejaa ujumbe kwa mashabiki wake bila kuangalia umri hivyo anawaomba wampe sapoti ya kutosha katika kazi hiyo na zinazofuata.

Best Nasso alisema kibao hicho ni muendelezo wa kuwapa burudani mashabiki wake ambapo ametamba na vibao vingi kikiwemo cha ‘Narudi kijijini’ ambacho kiliishika tasnia ya muziki wa kizazi kipya.

No comments:

Post a Comment

Pages