January 25, 2013

KAMATI YA BUNGE YA VIWANDA NA BIASHARA YATEMBELEA VIWANDA VYA KONYAGI NA TBL DAR

 Mjumbe wa Kamati ya Bunge ya Viwanda  na Biashara, Deo Sanga (kulia), akipata maelezo kutoka kwa Mkurugenzi Mtendaji wa Kiwanda cha Konyagi cha Tanzania Distilleries Limited (TDL), David Mgwassa,kuhusu utengenezaji wa konyagi kubwa wakati wa ziara ya kamati hiyo, kwenye kiwanda hicho, Dar es Salaam juzi.
 Wajumbe wa Kamati ya Bunge ya Viwanda na Biashara, wakiangalia uzalishaji walipotembelea kiwanda cha Konyagi cha Tanzania Distilleries Limited (TDL), Dar es Salaam
 Mwenyekiti wa Kamati ya Bunge ya Viwanda na Biashara, Mahamoud Mgimwa (kushoto) akizungumza na Mkurugenzi Mtendaji wa Kiwanda cha Konyagi cha Tanzania Distilleries Limited (TDL), David Mgwassa wakati wajumbe wa kamati hiyo walipotembelea kiwanda hicho Dar es Salaam.
Wajumbe wa Kamati ya Bunge ya Viwanda na Biashara, wakiangalia uzalishaji walipotembelea kiwanda cha Konyagi cha Tanzania Distilleries Limited (TDL), ares SDalaam
 Wajumbe wa Kamati ya Bunge ya Viwanda na Biashara wakitembelea sehemu ya mitambo ya kujaza bia kwenye chupa katika kiwanda cha TBL, Dar es Salaam
 Meneja wa Kiwanda cha Bia cha Kampuni ya Bia Tanzania, Martine Calvin (kulia), akiwapatia maelezo kuhusu historia ya kiwanda hicho, wajumbe wa Kamati ya Bunge ya Viwanda na Biashara, walipotembelea kiwanda hicho
 Baadhi ya wajumbe wa Kamati ya Bunge ya Viwanda na Biashara, wakipita eneo la matanki ya uchachuaji wa bia walipotembelea kiwanda cha Kampuni ya Bia Tanzania (TBL), juzi katika Makao Makuu kampuni hiyo, Dar es Salaam.

 Ofisa Uhusiano wa TBL, Doris Malulu (kulia) akiwakaribisha wajumbe wa kamati hiyo kwenye chumba cha mikutano tayari kupata taarifa ya utendaji wa kampuni hiyo.
 Mkurugenzi wa Miradi Maalumu wa Kampuni ya Bia Tanzania (TBL), Phocas Lasway akitoa maelezo jinsi ongezeko la kodi ya asilimia 25 lililovyoathiri uzalishaji wa kampuni hiyo.
 Mwenyekiti wa kamati hiyo, Mgimwa akielezea jinsi watakavyoshirikiana na TBL kutafuta ufumbuzi wa changamoto mbalimbali zinazikabili kampuni hiyo.Kushoto ni Katibu Mkuu wa Wizara ya Viwanda na Biashara, Joyce Mapunjo.
Katibu Mkuu wa Wizara ya Viwanda na Biashara, Joyce Mapunjo (kushoto), ambaye pia ni mjumbe wa Bodi ya Wakurugenzi wa Kampuni ya Bia Tanzania (TBL), akizungumza wakati wajumbe wa Kamati ya Bunge ya Viwanda na Biashara walipotembelea kiwanda cha Kampuni ya Bia Tanzania (TBL), juzi katika Makao Makuu kampuni hiyo, Dar es Salaam. Kutoka kulia ni Mjumbe wa kamati hiyo,  Ahmed Salum na Mahamoud Mgimwa ambaye ni mwenyekiti wa kamati hiyo.
 Mkurugenzi wa Maendeleo ya Wanachama na Mawasiliano wa CTI, Neema Mhondo akielezea jinsi Kikosi cha Zimamoto na Uokoaji kilivyopandisha kiholela ada kwa kampuni mbalimbali kutoka sh. 400,000 hadi milioni 7 kwa mwaka.
Wajumbe wa Kamati hiyo ya Bunge wakiwa katika picha ya pamoja baada ya kumaliza ziara kiwandani hapo. PICHA ZOTE NA KAMANDA WA MATUKIO BLOG

No comments:

Post a Comment

Pages