January 12, 2013

MAZINGIRA MAGUMU YA KUFANYIA KAZI SI SABABU YA MATOKEO MABAYA YA KAZI


Hii Bonge la Tripod Stand, ili iweze kupatikana kazi nzuri na matokeo bora ya kazi hata kama Bosi haelewi maana ya kitendea kazi kinachohitajika mahala kama hapa. Askari Magereza ambaye hakuweza kufahamika jina lake akimsaidia mdada huyu aliyekuwa akinasa matukio ya picha katika sherehe za mapinduzi, mjini Zanziba leo mchana, haikuweza kufahamika kama jamaa hawa walikuwa ni wanahabari au ni kutoka kwa bosi mmoja. Lakini mwisho wa siku Bosi anahitaji kazi iliyo nzuri bila kujali kuwa watendaji wake wanataabika katika kufanya kazi bila kuwa na vitendea kazi bora vinavyokwenda na wakati, na suala hili si kwa hawa jamaa pekee ila ni katika Ofisi nyingi tu hususan Vyombo vya habari vya hapa nchini. http://sufianimafoto.blogspot.com

No comments:

Post a Comment

Pages