January 13, 2013

MTOTO WA SHEIKH YAHYA AIBUKA NA KUPINGA RAIS AJAE KUWA MWANAMKE


DAR ES SALAAM, Tanzania

MAALIM Hassan Yahya Hussein, amepinga kauli iliyotolewa hivi karibuni na mtabiri mwenzake kuwa rais wa mwaka 2015 kuwa atakuwa mwanamke.

Akizungumza na wandishi wa habari jijini Dar es Salaam leo kuhusu utabiri wake wa matukio yatakayotokea mwaka 2013, ambapo mwaka huo utaanza  Machi 21 mwaka huu.

Maalim Hussein alisema kiutabiri huwezi kutoa utabiri katika matukio ya mwaka mmoja mbele, kitendo cha mtabiri huyo ni sawa na kuwakatisha tamaa baadhi ya watu wenye nia ya kutaka kugombea nafasi hiyo mwaka 2015.

“Huwezi kutoa utabiri wa miaka miwili mbele hata Sheikh Yahya Hussein mtabiri aliyekuwa akikubalika hakuwahi kufanya hivyo, pia sikubaliani naye kuwa rais ajaye atakuwa mwanamke hata ukiangalia katika njia zetu za utabiri ambazo ni namba zinapingana na hilo”alisema.

Alisema matokeo ya utabiri kama huo ni sawa na uwamuzi wa kuwafungia milango kidemokrasia baadhi ya wanasiasa wenye nia ya kugombea urais mwaka 2015.

“Kuna baadhi ya viongozi wakiwemo Lowassa na Membe wanadaiwa kuwa huenda wakagombea nafasi hiyo, kwa kufanya hivyo itakuwa ni kuwakatisha tamaa”alisema.

Akizungumzia utabiri wa mwaka huu, alisema kuwa kuna viongozi wengi, wabunge, wakuu wa mikoa na wengine watatoa matamshi ya  utatanishi na kusababisha hofu na mitafaruku itakayowafanya watu kupigana.

 Vile vile alisema wapo wabunge katika Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania wataungana katika masuala ya msingi yatakayohusu utaifa bila kujali itikadi zao za kivyama au kimajimbo.

Maalim Hussein alibainisha kuwa Rais Jakaya Kikwete ataunganisha nchi na kuwa moja yenye uimara wa utaifa kuliko watangulizi wake, akishirikiana zaidi na wanasiasa na viongozi wa dini kuondoa mtikisiko wa uvunjifu wa amani uliyojitokea mwaka jana.

Aidha, Chama kimoja cha siasa kitajitokeza na kitachochea kujitenga na kuunda Taifa lake hata hivyo, kusudio hilo halitafanikiwa kwani litapingwa na Watanzania wote kwa kauli moja na vitendo.

Maalim Hussein pia alisema kutatokea vifo vya ghafla kwa watunzi wa hadithi na vitabu, wandishi wa habari, wanasiasa na wasanii ambapo matukio hayo yatakuwa mabaya zaidi kuliko mwaka jana. 


Akigusia Uchaguzi Mkuu utakaofanyika hivi karibuni   nchini Kenya ambao ni majirani, alisema kuwa Muungano wa CORD, ukiongozwa na Raila Odinga utashinda uchaguzi huo, ambao ana amini utakuwa wa amani na tulivu.

“Ushindi huo utakuja baada ya kuushinda Muungano wa Jubilee ukiongozwa na akina Uhuru Kenyata na Ruto pamoja na ule wa Musalia Mudavadi unaoitwa AMANI”alisema.

2 comments:

Pages