January 06, 2013

PRINCESS YA WOLPER KUTOKA HIVI KARIBUNI


Na Elizabeth John
NYOTA wa filamu nchini, Jacline Wolper anajipanga kusambaza kazi yake mpya inayokwenda kwa jina la ‘Princess’, hivi karibuni.

Akizungumza jijini Dar es Salaam, Wolper alisema yupo katika hatua za mwisho za uandaaji wa kazi hiyo ambayo anamini itakuwa gumzo mtaani kutokana na stori ambayo ameielezea ndani yake.

Alisema anawaomba wadau wa kazi zake wakae mkao wa kula kwaajili ya kazi hiyo ambayo anatarajia kuisambaza hivi karibuni.

“Namshukuru mungu maandalizi ya kazi yangu yameenda vizuri na hadi sasa ndio namalizia kazi hii, wapenzi wa kazi zangu wake vizuri kwaajili ya kuipokea kazi hii ambayo imefuata maadili ya mtoto wa kitanzania,” alisema Wolper.

Alisema yeye ni Mtanzania hivyo ameamua kufanya kitu ambacho kipo katika jamii inayomzunguka na kuelimisha kwa uwezo aliokuwa nao yeye.

No comments:

Post a Comment

Pages