January 02, 2013

USAJILI WA THIERRY HENRY WAOTA MBAWA ARSENAL

LONDON, England

Wenger Mfaransa aliyeratibu na kukaribia kupata saini ya pili ya mkopo ya nahodha wake wa zamani Thiery Henry, amekiri rasmi kushindwa kwa jaribio hilo na sasa wameachana na nia ya kumkopa Henry kutoa New York Red Bulls

WAKATI Washika Bunduki wakikabwa koo na kulazimishwa sarte ya bao 1-1 na Southamton, kocha wa Arsenal, Arsene Wenger amekiri rasmi kushindwa kwa jaribio lake la kumchukua kwa mkopo nahodha wa zamani wa klabu hiyo Thierry Henry.

Mwishoni mwa Desemba, Gunners ilikuwa na matumaini makubwa ya kupata saini ya mkopo ya mpachika mabao anayeshikilia rekodi ya klabu hiyo, Henry, 35, akitokea klabu yake ya New York Red Bulls ya Marekani katika usajili wa majira ya baridi ulioanza Januari 1.

Lakini Wenger alisema: “Yeye hayuko tayari na pia hajarejea kutoka mapumzikoni kwa vyovyote. Kwa sasa hatuna tena muda wa kushughulikia hilo.”

Jaribio hili linaloshindwa rasmi ni la pili kwa Wenger kumtwaa kwa mkopo Henry, ambaye anashikilia rekodi ya kuifungia Gunners mabao 228 katika mechi 337 alizocheza.

Henry ilionekana kama aliyekaribia kumalizana na Gunners – huku akichangia kukubali nyongeza ya mkataba mpya wa kubaki Emirates kwa mshambuliaji Theo Walcott.

Akizungumzia mechi ya sare ya 1-1 na Southampton, Wenger alisema kikosi chake kilistahili kupoteza pointi mbili na kwamba kuna kila sababu ya kuangalia njia mbadala za kukiimarisha kikosi katika usajili wa Januari.

Na wakati alipoonekana kutaka kujiimarisha Januria hii na kuulizwa kama anaweza jkufanya usajili wowote, Wenger alisema: “Ndiyo, nitakuwa kazini. 

“Tutaangalia kila kona, kila mahali, tumeamua kuwa wazi kabisa. Tunahitaji kuongeza nguvu ya kikosi chetu,” alitamba Wenger, anayehaha kwa misimu minane sasa kusaka taji bila mafanikio.

No comments:

Post a Comment

Pages