January 11, 2013

UZINDUZI WA MRADI WA "ONE WORLD FOOTBALL FOR AFRICA"

  Baadhi ya Watoto wakibeba mabango yenye ujumbe tofauti unaosisitiza kulindwa haki zao,wakipita kwa
maandamano mbele ya Mgeni rasmi Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein,katika sherehe za  uzinduzi wa Mradi wa  "ONE WORLD FOOTBALL FOR AFRICA", zilizofanyika jana katika Uwanja wa Amaan Studiuam,ikiwa ni shamra shamra za Miaka 49 ya Mapinduzi Matukufu ya Zanzibar. (Picha na Ramadhan Othman,Ikulu)

 Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein,akiwapungia Mkono Vijana waliopita mbele ya Jukwaa la Uwanja wa Amaan Studiuam,akipokea maandamano ya vijana katika sherehe za  uzinduzi wa Mradi wa  "ONE WORLD FOOTBALL FOR AFRICA", ikiwa ni shamra shamra za Miaka 49 ya Mapinduzi Matukufu ya Zanzibar,(kulia) ni Waziri wa Habari,Utalii,Utamaduni na MIchezo Said Ali Mbarouk.(Picha na Ramadhan Othman,Ikulu)
 Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein,akitia saini Mpira katika uzinduzi wa Mradi wa  "ONE WORLD FOOTBALL FOR AFRICA",mradi ambao utawapatia vijana wa Zanzibar Mipira Ishirini Elfu ,(20,000) katika vikundi mbali mbali na kupelekea kuongezeka kwa vipaji vya Soka nchini,katika sherhe za kuadhimisha miaka 49 ya mapinduzi Matukufu ya Zanzibar.(Picha na Ramadhan Othman,Ikulu)
 Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein,akipokea kitabu kutoka kwa Nasra Sheikh Mohamed,wa Skuli ya Mwembeshauri Mjini Unguja,kitabu  chenye Agenda ya Watoto kuhusu usisitizaji kwa Serikali na Jamii kushirikiana katika kuwapatia haki zao za Msingi bila unyanyasaji. katika uzinduzi wa Mradi wa  "ONE WORLD FOOTBALL FOR AFRICA",katika uwanja wa Amaan Studium ikiwa ni shamra shamra za Miaka 49 ya Mapinduzi Matukufu ya Zanzibar. (Picha na Ramadhan Othman,Ikulu)

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein,akimkabidhi zawadi Mwakilishi wa Shirika la UNICEF Paulo Edwards, katika sherehe za uzinduzi wa Mradi wa ONE WORLD FOOTBALL FOR AFRICA" ,katika  Uwanja wa Amaan Studium, ikiwa ni shamra shamra za Miaka 49 ya Mapinduzi Matukufu ya Zanzibar. (Picha na Ramadhan Othman,Ikulu)

No comments:

Post a Comment

Pages