January 04, 2013

VENUS WILLIAMS AJIPA MATUMAINI AUSTRALIAN OPEN


NEW YORK, Marekani

MCHEZAJI Venus Williams anaamini ameiva tayari kwa kuonesha kiwango katika michuano ya mwezi huu ya Australian Open, baada ya kufanya vema bila kichapo katika michuano ya nyota mmoja mmoja ya Kombe la Hopman.

Williams alikuwa na michuano ya aina yake ya Kombe la Hopman, alikomshinda Mhispania Anabel Medina Garrigues kwa seti mfululizo Alhamisi kukamilisha mechi tatu za nyota mmoja mmoja alizocheza.

Lakini Mmarekani huyo anaamini kuwa kutwaa ubingwa wa Hopman kutamsukuma kupata mafanikio, michuano ambayo nyota mwenzake wa timu ya taifa John Isner alijitoa katika michuano hiyo mapema katika siku ya kwanza kwa matatizo ya goti.

Nyota huyo mwenye miaka 32, alikuwa na matumaini ya kupata mechi moja ya mchezaji mmoja mmoja Jumamosi, kabla ya kupaa zake jijini Melbourne kupigania kutwaa Grand Slam ya kwanza kwa mwaka huu wa 2013, katika michuano itakayoanza Januari 14.

Williams, ambaye hajawahi kuvuka raundi ya nne katika kuwania Grand Slam, tangu alipofanya hivyo mwaka 2010 kwenye US Open, ameonekana kuimarika kiwango kama alivyoonekana katika Kombe la Hopman.

No comments:

Post a Comment

Pages