January 19, 2013

WALCOTT AJIFUNGA MIAKA MITATU GUNNERS


LONDON, England

Wenger alikuwa katika wasiwasi mkubwa wa kumpoteza mkali huyo, kama ilivyokuwa kwa kina Cesc Fabregas, Samir Nasri, Robin van Persie na Alex Song waliotimka zao katika kipindi cha majira ya joto ya miaka miwili iliyopita

WINGA hatari wa kimataifa wa England, Theo Walcott hatimaye amesaini mkataba mpya wa kuendelea kuichezea Arsenal.

Walcott, 23, alikamilisha usajili huo jana kwa kurefuisha mkataba wake kwa miaka mitatu na nusu utakaomuwezesha kupokea mshahara wa pauni 100,000 kwa wiki akiwa na klabu hiyo ya Emirates.

Jioni ya juzi Alihamisi bosi wake Arsene Wenger alithibitisha: “Nina matumaini makubwa ya kumsainisha mkataba huo kabla ya mwisho wa wiki. Kuna uwezekano mkubwa wa kufanyika hilo. Matumaini niliyonayo juu ya ukamilifu wa hilo ni asilimia 99 sasa.”

Wenger alikuwa katika wasiwasi mkubwa wa kumpoteza mkali huyo wa safu ya mbele kama ilivyomtokea kwa nyota kadhaa klabuni Emirates, baada ya mktaba wake kuelekea ukingoni huku akigoma kusaini mpya akishinikiza ongezeko la mshahara wake.

Tayari huko nyuma bosi huyo wa Gunners alishashuhudia wakali wake kama Cesc Fabregas, Samir Nasri, Robin van Persie na Alex Song wakitimka zao katika kipindi cha majira ya joto ya miaka miwili iliyopita.

Na Wenger hakuficha ukweli juu ya hilo, ambapo alikiri: “Ndio nilikuwa na wasiwasi sana wa kumpoteza, kwamba angeweza kuondoka Emirates kwa sababu nina uzoefu wa kutosha wa aina ya mazungumzo na makubaliano tuliyokuwa tukifanya na yeye.

“Wakati jambo moja linapodumu kwa muda mrefu kwenye majadiliano, kamwe hilo halina ishara nzuri kimatokeo.

“Na ilituichukua muda mrefu kutufikisha pale sisi tulipotaka kufika kimazungumzo kutuwezesha kupata tulichohitaji. Hili halijamaliziika rasmi, lakini nina matumaini makubwa ya kulimaliza hilo wikiendi hii.”

Kukamilika kwa usajili wa Walcott aliyekuwa akiwindwa na klabu kadhaa za England na nje ya nchi hiyo, kunampa fursa Wenger ya kugeukia soko la usajili wa majira ya baridi baranmi Ulaya, lililofunguliwa Januari 1.

……….The Sun/Daily Mail………..

No comments:

Post a Comment

Pages