January 10, 2013

Z ANTO KUTOKA NA NGOMA KALI


Na Elizabeth John
NYOTA wa muziki wa bongo fleva nchini, Ally Mohamed ‘Z Anto’ amesema kwa mwaka huu amejipanga kurudi upya katika tasnia hiyo kutokana na kuwa na ngoma kali katika maktaba yake.

Akizungumza jijini Dar es Salaam, Z. Anto alisema ana azina kubwa ya nyimbo huku akiwa anatafakari ni nyimbo ipi aanze kuiachia kutokana na kila moja kuwa katika kiwango cha juu.

“Kwa sasa natakari namna nitakavyoachia nyimbo zangu kutokana na kila moja kuwa katika kiwango cha juu, hivyo najaribu kukaa na watu wangu wa karibu ili wanishauri ni nyimbo ipi ianze kwenda hewani na kufuata nyingine,” alisema Z.Anto.

Nyota huyo aliyezaliwa 1998 jijini Dar es Salaam aliwahi kutamba na nyimbo mbalimbali kama Kisiwa cha Malavidavi, Mpenzi Jini, Imani Sina, Mpenzi Spesho, Chakula Changu zilizompa umaarufu pamoja na mafanikio makubwa.

Z. Anto anawaomba mashabiki wake kukaa katika mkao wa kula wakisubiri kazi mpya ambazo zipo katika ubora wa hali ya juu kwa lengo la kuhakikisha anaridisha adhi ya awali ambapo alikuwa gumzo Afrika Mashariki.

“Mashabiki wangu wakae mkao wa kula kusubiri kazi zangu mpya ambazo ziko kwenye maktaba na wakati wowote baada ya kutafakari nitaamua nianze kuachia wimbo upi ili afanikishe kukonga nyoyo za wapenzi wa muziki wa kizazi kipya nchini,” alisema.

No comments:

Post a Comment

Pages