January 09, 2013

ZIARA YA SIKU NNE YA RAIS KIKWETE MKOANI TABORA

Rais Jakaya Kikwete akitoa maelekezo kwa Waziri wa Ujenzi Dk John Pombe Magufuli, Waziri wa Maji Profesa Jumanne Maghembe na Waziri wa Fedha Dk William Mgimwa, kabla hajahutubia mkutano mkubwa wa hadhara mjini Nzega katika ziara yake ya siku nne ya mkoa wa Tabora, ambapo anazindua miradi kadhaa ya maendeleo ikiwemo barabara, madaraja na maji.
Rais Kikwete akihutubia mkutano mkubwa wa hadhara mjini Nzega katika ziara yake ya siku nne ya mkoa wa Tabora ambapo anazindua miradi kadhaa ya maendeleo, ikiwamo ya barabara, madaraja na maji.
  Baddhi ya wananchi waliohudhuria mkutano wa hadhara wa Rais Kikwete.
Rais Kikwete akisikilia maelezo ya Meneja wa TANESCO wa Nzega akielezea mikakati ya kuwapatia wakazi wa hapo nishati hiyo, wakati wa mkutano mkubwa wa hadhara mjini Nzega katika ziara yake ya siku nne ya mkoa wa Tabora.
Rais Kikwete akipokea ripoti ya maendeleo ya Wilaya ya Uyui toka kwa Mkuu wa Wilaya hiyo, Mhe Lucy Mayenga wakati Rais alipowasili Tabora mjini kuendelea na ziara yake.
Rais Kikwete akipokea ripoti ya maendeleo ya Wilaya ya Tabora Mjini toka kwa Mkuu wa Wilaya hiyo Suleiman Kumchaya, wakati Rais alipowasili Tabora mjini kuendelea na ziara yake ya siku nne.
Rais Kikwete akipata maelzo ya ujenzi wa barabara ya Tabora-Ndono kabla hajazindua rasmi i ujenzi wa  barabara hiyo akiwa katika ziara yake ya siku nne
Rais Kikwete akikata utepe kuzindua rasmi  ujenzi wa barabara hiyo.

No comments:

Post a Comment

Pages