January 10, 2013

Nyota wa Seattle Sounders FC kuendesha semina ya soka nchini


Na Mwandishi wetu
WAWAKILISHI wawili wa klabu ya Seattle Sounders ya Marekani  wataendesha semina kwa wadau wa michezo  hapa nchini katika ziara yao ya siku tisa kuanzia leo.
Wawakilishi hao ni beki wa timu hiyo, Marc Burch na kipa aliyestaafu  ambaye kwa sasa ni mtangazaji , Kasey Keller .
Wakiwa nchini, wachezaji hao wataendesha semina kwa vilabu vya Ligi Kuu ya Tanzania Bara na shule za msingi katika siku na muda ambao  utangazwa hapo baadaye. Z
iara hiyo ni moja ya kukuza ushirikiano baina ya Seattle Sounders na  wadau wa michezo nchini na ikumbukwe kuwa timu hiyo iliwahi kumchukua mchezaji nyota wa Tanzania, Mrisho Ngassa kucheza mechi ya kihistoria dhidi ya timu ya Manchester United.
Kwa kushirikiana na Washington Global Health Alliance (WGHA),  wawakilsihi wa timu hiyo pia watatembelea miradi mitatu ya upande wa afya iliyopo mkoani Arusha  ikiwa pamoja na World Vision, taasisu ya PATH  na Chuo kijulikanacho kwa jina la Washington State University's Paul G. Allen School for Global Animal.
 "Ziara hii itadumisha na kuhimarisha uhusiano wetu na serikali ya Tanzania, “ alisema Mmiliki wa timu hiyo, Joe Roth ambaye pia alisema Kesey na March watakuwa mabalozi wakubwa wa timu yao katika ziara hiyo.
Alisema kuwa wajumbe hao pia watatembelea vivutio vya utalii kama Ngorongoro Crater na jiji kubwa la Tanzania, Dar es Salaam. Timu hiyo ya Marekani iliingia katika ushirikiano na WGHA mwaka 2009. Mpango huo una lengo la kushughulika na masuala ya afya kwa binadamu nchini na Kimataifa.

No comments:

Post a Comment

Pages