March 27, 2013

HISPANIA YAIZABUA UFARANSA NYUMBANI STADE de FRANCE

 Paul Pogba wa Ufaransa, akimrukia na kumshika kiungo wa Hispania, Xabi Alonso, tukio ambalo lilimfanya aoneshwe kadi ya pili ya njano na kupigwa 'red-card' iliyomtoa nje ya uwanja kunako dakika ya 78 ya pambano la kuwania kufuzu Kombe la Dunia 2014, lililoisha kwa Hispania kuwachapa wenyeji Ufaransa bao 1-0 kwenye dimba la Stade de France jijini Paris usiku wa kuamkia leo.
 Kiungo Xavi Hernandez wa Hispania akionywa kwa kadi ya njano na mwamuzi Viktor Kassai wa Hungary katika mechi ya kuwania kufuzu Kombe la Dunia 2014 kati ya Ufaransa na Hispania.
 Paul Pogba wa Ufaransa (wa pili kulia mwenye jezi namba 19), akioneshwa 'red-card' iliyomtoa nje ya uwanja katika dakika ya 78 ya pambano la kuwania kufuzu Kombe la Dunia 2014, lililoisha kwa Hispania kuwachapa wenyeji Ufaransa bao 1-0 kwenye dimba la Stade de France jijini Paris usiku wa kuamkia leo.
 Mshambuliaji wa Ufaransa, Karim Benzema (katikati) akitafuta mbinu za kuwatoka wachezaji wa timu ya taifa ya Hispania katika mechi baina ya nchi hizo jana usiku.
 Mlinda mlango wa Ufaransa, Hugo Lloris (kushoto) akijaribu kuokoa mpira wa Pedro usitinge katika nyavu zake. Jitihada ambazo hazikuzaa matunda, hivyo mpira kutinga nyavuni kuandika bao pekee la Hispania. 
 Kipa Hugo Lloris akiukodolea macho mpira uliopigwa na Pedro ukitinga nyavuni kuiandikia Hispania bao pekee katika mechi ya kuwania kufuzu Kombe la Dunia 2014.
 Pedro akishangilia bao hilo.
 Hii ilikuwa ni mapema kabla ya kutolewa kwa kadi nyekundu, Paul Pogba akichuana na viungo bora na mahiri duniani wa timu ya taifa ya Hispania, Xavi na Andres Iniesta.
Kipa wa Hispania, Victor Valdes, akijiandaa kuzuia shuti la winga wa Ufaransa, Frank Ribery, huku beki Gerrard Pique akiwa tayari kumsaidia.
Beki wa kushoto wa Ufaransa, Patrice Evra (kulia) akizuia shuti jepesi la mshambuliaji David Villa wa Hispania.

No comments:

Post a Comment

Pages