KATIBU Mkuu wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Jimbo la Ukonga, Jumaa Mwipopo, ameitaka Serikali kuhakikisha kuwa inawapatia msaada
waathirika wa kimbunga kilichotokea Kata ya Majohe wilayani Ilala, Machi 3 mwaka huu.
Katibu alisema hayo jijini
Dar es Salaam jana, alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari kuhusu kitendo
cha Halmashauri hiyo kukaa kimya hadi leo kwa kutopeleka msaada tangu kutokea
kwa tukio hilo.
Mwipopo alisema kimbuka
hicho cha upepo kilichotokana na mvua kubwa kilisababisha kubomoka nyumba
zipatazo 176 katika mitaa ya Nyeburu, Zavala na Kigenzi katika kata hiyo.
Alisema wanatoa siku saba
kuiomba Halmashauri hiyo na serikali kuwa inawapatia misaada ya chakula ikiwa ni pamoja
na kuwajengaewa makazi yao, hawana uwezo wa kujenga, ili warudi katika maisha
yao ya kawaida kama wengine.
Mwipopo alisema endapo
itashindikana basi wataitisha mkutano ili wa waeleze wakazi hao wa Nyeburu na
Zavala kuwa serikali yao imeshindwa kuwasaidia ama huenda ikawa inawachukulia
kuwa wao si sehemu ya Watanzania hivyo hawana haki ya kupata msaada.
“Inasikitisha kutokana na
kubaguliwa na kutowapa msaada wowote yakaribia mwezi sasa, wakati waathirika wa
mabomu Mbagala Waziri Mkuu alichangasha fedha kwa kuwaita wakurugenzi wa
Halmashauri na Mameya na kuwaamuru wachangie milioni 20 kila halmashauri kwa
ajili ya waathirika wa Mbagala na yetu ilitoa fedha hizo iweje kwetu
ishindikane”alisema Mwipopo.
Mwipopo alifafanua kuwa
mwaka 2012/13, zilitengwa fedha katika ofisi ya Meya kwa ajili ya misaada kwa
jamii, zilitengwa jumla ya milioni 21.8 ambako kazi yake ni kwa ajili ya
majanga kama haya yanapotokea.
Aidha, taarifa yao hiyo
imesambazwa kwenye Ofisi ya Waziri Mkuu, Katibu Mkuu wa Chedema Taifa, Mkuu wa
Mkoa, Mkuu wa Wilaya na Meya wa Manispaa ya Ilala.
Ni hivi karibuni Mkuu wa
Mkoa alisikika kuna matatizo mengine yakondani ya uwezo wao wanachi, kwani kama
serikali ikiyaendekeza itajikuta mwaka mzima ifanyakazi hiyo.
No comments:
Post a Comment