HABARI MSETO (HEADER)


Breaking

March 20, 2013

KINANA AZUNGUMZA NA WAZIRI ANAYESHUGHULIKIA MASUALA YA CPC CHINA, ATEMBELEA CHINALCO LEO

  KATIBU Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana akisalimiana na Waziri anayeshughulikia mambo ya chama katika Chama Cha Kikomunisti cha China, Wang Jiarui, alipokutana naye leo Machi 20, 2013, kwenye Ofisi za CPC, mjini Beijing, China na kuwa na mazungumzo naye. Nyuma ya Kinana ni Naibu Katibu Mkuu wa CCM (Zanzibar) Vuai Ali Vuai. (Picha na Bashir Nkoromo).
 Katibu Mkuu wa CCM Abdulrahman Kinana (kulia) akitazama baadhi ya malighafi, alipotembelea kampuni ya Aluminum ya China (CHINALCO), alipotembelea kiwanda hicho mjini Beijing,  Machi 20, 2013. Wapili kulia ni Rais wa Kampuni hiyo Xiong Weiping.
 Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana, akizungumza na waziri anayeshughulikia masuala ya chama wa Chama cha Kikomnisti cha China, Wang Jiarui, alipokutana naye leo Machi 20, 2013, kwenye Ofisi za CPC, mjini Beijing, China.
  Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana akitia saini kweneye kitabu maalum cha wageni, katika kampuni ya Aluminum ya China ((CHINALCO). Kushoto ni Rais wa Kampuni hiyo, Xiong Weiping na wapili kushoto ni Katibu wa Jumuia ya Wazazi Tanzania, Khamis Suleiman Dadi.
 Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana na ujumbe wake wakiwa katika mazungumzo na uongozi wa CHINALCO, Kinana na ujumbe huo walipotembelea kampuni hiyo wakiwa katika ziara ya mafunzo Beijing, China.
 . Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana akimpa zwadi ya kinyagoo cha Kimakonde cha aina ya 'Ujamaa', Rais wa kampuni ya Aluminum ya China (CHINALCO) kilichopo mjini Beijing, Xiong Weiping, alipotembelea kampuni hiyo na ujumbe wa viongozi 14 wa CCM ambao yupo nao katika ziara ya mafunzo nchini China. 
Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana akipewa zwadi ya pambo la Kichina, na  Rais wa kampuni ya Aluminum ya China (CHINALCO) kilichopo mjini Beijing, Xiong Weiping, Kinana alipotembelea kampuni hiyo na ujumbe wa viongozi 14 wa CCM ambao yupo nao katika ziara ya mafunzo nchini China. Kulia ni Katibu wa NEC, Siasa na Uhusiano wa Kimataifa, Dk. Asha-Rose Migiro.

No comments:

Post a Comment

Pages