UTT
AMIS ni taasisi ya Serikali ya Tanzania iliyo chini ya Wizara ya Fedha
ambayo dhumuni lake kuu ni kuanzisha na kuendesha mifuko ya uwekezaji wa
pamoja hapa nchini ili kuwawezesha wananchi wengi zaidi kujiwekea akiba
na kuwekeza katika masoko ya fedha na mitaji.
Changamoto
kubwa iliyopo ni kwamba bado hali ya utamaduni wa kuweka akiba na
kuwekeza katika masoko ya fedha na mitaji bado iko chini kwa sababu za
kihistoria, kijamii, kiuchumi na wakati mwingine sababu huwa ni kipato
kidogo na mahitaji ni mengi. Ukweli unabaki ya kuwa hakuna siku fedha
zinaweza kutosha.
Hivyo inamlazimu kujenga nidhamu na tabia ya kujiwekea akiba ya fedha kutokana na kipato anachapata.
Siyo
jambo rahisi kuweza kuweka akiba ya fedha, lakini ili uweze kufanya
hivyo ni muhimu kujenga nidhamu katika matumizi yetu.
Afisa Masoko na
Uhusiano wa UTT AMIS, Rahim Mwanga anasema “Suala si kuweka akiba na
kuwekeza tuu, ila tunatakiwa kuweka akiba na kuwekeza kwa ufanisi ambao
ni Uwekezaji unaozingatia kuwa na malengo, kuweka mpango wa kufikia
malengo na muda. Mfano lengo ni kuwa na milioni 5, kwa muda wa miaka 3
na utawekeza kila mwezi. Hiyo ndiyo itakayo kuwa dira ya kukuwezesha
kufika malengo.
Afisa Masoko na Uhusiano wa UTT
AMIS, Rahim Mwanga anasema, "Siku zote ukiwa na akiba ya fedha unatakiwa
kuziwekeza. Uwekezaji ni dhana pana, kwa mfano, mwingine anataka
kununua kiwanja, mwingine aanzishe biashara, mwingine ampeleke mtoto
shule, mwingine akasome yeye mwenyewe, lengo likiwa ni kwamba ile fedha
ya akiba ilete matokeo chanya kwake. Hata hivyo, inatakiwa ieleweke
kwamba kuna muda kati ya kuweka akiba, kuwekeza na kutimiza lengo.
Kwa
mfano, ninataka kuweka akiba kwa ajili ya elimu ya mwanangu ambaye ana
mwaka mmoja sasa, kwa hiyo kuna miaka miwili au mitatu baadaye aanze
chekechea, kwa hiyo nikiweka akiba tu katika sehemu ambayo haikuwi
katika miaka mitatu hiyo maana yake itakuwa haina tija kwa sababu hapo
katikati lazima kutakuwa na mfumuko wa bei na mambo mengine, kwa hiyo
kinachotakiwa ni kuwekeza fedha hizo za akiba kabla ya kuja kufanya
uwekezaji wa kumpeleka mtoto shule.
Kwa hiyo hapa
katikati niwekeze wapi sehemu ambayo ipo salama au itanipa tija nzuri na
haitanihitaji kuhangaika sana. Sasa sehemu hizi watu wengi
hawajazichangamkia. Sehemu hizo ni katika masoko ya fedha na masoko ya
mitaji."
Anasema, "Tunapozungumzia masoko ya mitaji
mfano wake ni Soko la Hisa la Dar es Salaam (DSE), kwani katika soko
hili kuna makampuni yamejiorodhesha yakiuza mitaji na kutafuta mitaji
kwa kuuza hisa, kwa hiyo ni sehemu mojawapo ambayo watu wanaweza kwenda
kuwekeza pia katika dhamana za serikali za muda mrefu.
Dhamana
za kapuni(Corporate bonds) na katika Vipande. Sehemu nyingine ni katika
masoko ya fedha huku kuna akaunti za muda maalumu (fixed deposit
accounts) na akaunti ambazo hazina muda maalumu (call deposit accounts),
pia kuna dhamana za Serikali.
Mwekezaji anaweza
kuwekeza moja kwa moja katika dhamana hizo hapo juu, lakini kuna
changamoto za mwekezaji mmoja mmoja kufikia soko na kunufaika
kikamilifu, kama vile elimu ya kutosha, urahisi wa kuwekeza na kutoka na
faida nzuri.
Lakini kupitia UTT AMIS changamoto
hizo zinapungua kupitia kuwekeza kwenye mifuko ya uwekezaji wa pamoja.
Mifuko ya uwekezaji wa pamoja ni fursa inayomuwezesha mtu mmoja mmoja au
taasisi, kampuni kuwekeza rasilimali fedha zao kupitia UTT AMIS(Meneja)
na UTT AMIS kazi yetu ni kuwekeza kwa niaba yao yaani mtu mmoja mmoja,
taasisi au makampuni katika dhamana hizo kulingana na sera ya Uwekezaji
ya mfuko."
Anasema, " Umiliki wa Uwekezaji katika
katika mfuko wa uwekezaji wa pamoja huitwa kipande (unit). Miongoni ya
faida kubwa ambayo mwekezaji anaipata kwa kujiunga na mifuko ya
uwekezaji wa pamoja badala ya kuwekeza mmoja mmoja katika masoko ya
fedha na masoko ya mitaji ni faida shindani ukilinganisha na baadhi ya
bidhaa za aina hiyo sokoni."
Mwanga anasema, "Kwa
mfano, katika benki tukitumia akaunti ya muda maalumu (fixed deposit
accounts), katika akaunti hii benki inamlipa mwekekezaji anayewekeza
katika akaunti hiyo kulingana na muda na kiasi anachowekeza na kiwango
cha chini cha kuwekeza katika benki ni milioni moja au laki tano.
Kwa
mwaka huwa benki zinatoa riba ya asilimia tatu hadi sita au saba,
lakini kama ukiwekeza kiasi kikubwa katika mabenki unakuwa katika nafasi
ya kupata riba nzuri, kwa mfano kuanzia milioni 500 na kuendelea
unaweza kupata riba ya kuanzia asilimia 10 hadi 11 kulingana na kiwango
cha fedha , uhitaji wa ukwasi wa benki na hali ya uchumi."
Anasema,
"Hapo ndipo inapokuja dhana ya uwekezaji wa pamoja, kwamba kila mtu
kutokana na uwezo wake anaweza kupeleka fedha katika mfuko na hivyo kwa
pamoja meneja wa mfuko yaani UTT AMIS kuwa na kiwango kikubwa. Kwa mfano
kikifika kiwango cha bilioni 2, mfuko unakuwa na uwezo wa kuweza
kuzungumza na benki na kupata riba nzuri.
Kwa
mfano benki inaweza kukubali kutokana na uwekezaji wa kiasi hicho cha
fedha na kutoa riba ya asilimia 10 kwa mwaka, kwa hiyo ina maana kila
aliyewekeza naye atafaidika kwa asilimia 10.
Yaani
aliyewekeza Sh 20,000 atatapata faida ya asilimia 10, aliyewekeza Sh.
30,000 atapata faida ya asilimia 10 na aliyewekeza 20 milioni atapata
faida ya asilimia 10."
Kwa kifupi ni kwamba, faida
ya kwanza ya dhana ya uwekezaji wa pamoja ni kuwawezesha wawekezaji
wadogo, wa kati na wawekezaji wakubwa kuweka nguvu pamoja na kuwekeza
ili kupata faida nzuri na shindani zaidi kuliko soko lingeweza kuwapa
wawekezaji mmoja mmoja.
Faida ya pili ambayo
wawekezaji wanaipata kwa kutumia mifuko ya uwekezaji wa pamoja ni
uwekezaji mseto. UTT AMIS inawekeza katika masoko ya fedha na masoko ya
mitaji, pia haiwekezi fedha zote katika kapu moja ili kuhakikisha
kunakuwa na usalama wa fedha za mwekezaji, kupata faida nzuri na ukwasi
(liquidity) yaani mtu akiihitaji fedha yake aweze kuipata kwa uharaka na
pia kwa uhakika.
Mwanga anasema, "Sasa ukiyatazama
masoko ya fedha na masoko ya mitaji utaona kwenye masoko ya mitaji
ambapo ndiyo kwenye hisa kunakuwa hakuna uhakika kwamba nikiwekeza
katika kampuni fulani mwisho wa mwaka nitapata faida kwa hiyo inategemea
na ufanisi ila faida ikipatikana huwa ni kubwa. Katika masoko ya fedha
faida siyo kubwa ila kuna uhakika wa kuipata hiyo faida."
Kwa
hiyo UTT AMIS inachokifanya ni kutawanya inachokipita, kwamba kama
wanapata Sh. 100 basi Sh. 60 wataipeleka katika sehemu salama zaidi
kwenye masoko ya fedha, yaani Sh 30 kwenye akaunti ya muda maalumu
(fixed deposit accounts), Sh 10 akaunti ambazo hazina muda malumu (call
deposit accounts), Sh. 10 treasury bills (dhamana za muda
mfupi), Sh 10 treasury bonds (dhamana za muda mrefu).
Sh
40 iliyobaki itatawanywa kwenye makampuni katika soko la hisa, yaani Sh
3 zitapelekwa labda DCB, Sh 8 TBL, Sh 10 TCC, Sh 4 Twiga. Kwa hiyo kama
kutatokea mdororo kwenye sehemu moja basi sehemu nyingine itaibeba
sehemu nyingine katika kuhakikisha usalama wa mali na ndiyo maana
uwekezaji unatawanywa.
Kampuni ya UTT AMIS
inasimamia mifuko sita ya uwekezaji wa pamoja ambayo ni Mfuko wa Umoja,
Mfuko wa Wekeza Maisha, Mfuko wa Watoto, Mfuko wa Kujikimu, Mfuko wa
Ukwasi na Mfuko wa Hati Fungani.
MFUKO WA UMOJA
Umoja ni mfuko wa wazi wenye uwiano sawa wa uwekezaji unaoufanya kuwa mfuko bora wenye hatari za uwekezaji wa kiwango cha kati.
Mfuko
wa Umoja unawekeza kiwango kisichozidi asilimia 50 ya fedha zake kwenye
hisa zilizoorodheshwa kwenye soko la hisa la Dar es salaam na asilimia
50 nyingine huwekezwa kwenye dhamana zenye kutoa mapato ya kudumu.
Sera
ya uwekezaji kwa upande mmoja ni mpango madhubuti uliowekwa na mfuko
ili kutawanya rasilimali zake. Kwa upande mwingine ni mpango mkakati na
ni kinga endapo eneo moja la uwekezaji likifanya vibaya.
Aidha, uwekezaji kwenye hisa huwekezwa kwa kiwango cha chini ikilinganishwa na eneo lenye mapato cha kudumu.
Ni
mfuko wa kwanza kuanzishwa na umekuwa sokoni tangu mwezi wa tano mwaka
2005. Kwasasa mfuko unathamani inayozidi bil. 291 na wawekezaji zaidi ya
95,000. Kwa muda mrefu sasa mfuko umekuwa ukitoa faida nzuri iliyo kati ya asilimia 10 mpaka 20 (baada ya makato ya kodi).
Mwekezaji
wa mfuko wa Umoja anaweza kuuza vipande vyake muda wowote, pesa
ataipata ndani ya siku kumi za kazi toka alipowasilisha maombi. Hakuna
kipindi cha kizuizi.
Gharama za kuuza vipande vya
mfuko ni asilimia 1 ya thamani ya kipande ambayo ni nafuu zaidi sokoni
kwa kulinganisha na asilimia 10 ya kodi atakayokatwa mteja anayetoa
fedha zake alizoweka kwenye akiba ya muda maalumu ya benki.
Tathmini ya thamani halisi ya mfuko itakokotolewa kila siku ya kazi na thamani ya kipande kutangazwa.
Usalama
wa fedha za mwekezaji ni mkubwa kwasababu mfuko unasimamiwa na taasisi
ya serikali yenye kuaminika. Pia mfuko unatoa faida shindani,ukwasi na
usalama kwa fedha za mwekezaji. Kwa kuzingatia
maelezo hayo, unaweza kuwekeza kiwango cha kawaida kabisa katika mfuko
wa Umoja na utawezeshwa kufuatilia maendeleo yake kwa ukaribu.
MFUKO WA UWEKEZA MAISHA
Wekeza
Maisha ni mfuko wa kwanza wa uwekezaji wa pamoja kuanzishwa na kampuni
ya UTT AMIS nchini wenye faida za bima ya maisha ndani yake.
Zaidi
ya asilimia 99 za fedha za wawekezaji wa mfuko wa Wekeza Maisha
huwekezwa kwenye masoko mbalimbali ya fedha na asilimia 1 kwa ajili ya
malipo ya bima.
Mambo muhimu kuhusu mfuko wa wekeza maisha.
Madhumuni:
Mfuko huu ni mpango wa wazi na wa muda mrefu unaokusudia kukuza mtaji
na kwa wakati huo huo kutoa kinga ya bima ya maisha, bima ya
ajali/ulemavu wa kudumu na gharama za mazishi.
Chaguo
la mpango wa uwekezaji: Mfuko unatoa fursa mbili za uwekezaji: (a)
Mpango wa Uwekezaji kwa Awamu na (b) uwekezaji wa mkupuo.
Nani anaruhusiwa Kuwekeza: Mfuko uko wazi kwa Mtanzania aliye ndani au nje ya nchi na awe mwenye umri kati ya miaka 18 hadi 55.
Ukomo wa Uwekezaji: Uanachama wa mwekezaji katika mfuko huu utakoma baada ya miaka 10.
Ukwasi: Uuzaji wa sehemu ya uwekezaji (vipande) katika mfuko) unaruhusiwa baada ya miaka mitano.
Thamani ya mwanzo ya kipande: Thamani ya mwanzo ya Kipande (face value) ilikuwa Sh.100.
Bei
ya kipande: Bei ya Kipande wakati wa mauzo ya mwanzo, yaani kuanzia
tarehe 16 Mei, 2007 hadi Julai 31, 2007 ilikuwa ni Sh.100/= na baada ya
hapo Kipande kinauzwa kulingana na thamani halisi. Mfano thamani ya bei
ya kipande kwa tarehe 31 mwezi wa nane ilikuwa ni sh. 719.1915.
Kiwango
cha kuwekeza: Kiwango cha chini kwa uwekezaji kwa miaka kumi ni Sh1
milioni na hakuna kiwango cha juu cha kuwekeza (isipokuwa mafao ya bima
ya maisha yatatolewa mpaka kufikia kiwango cha Sh 25 milioni tu).
Milioni
hii moja inaweza kuwekezwa kwa awamu au kwa mkupuo. Kiwango cha chini
cha uwekezaji wa awamu ni Sh.8,340/= kwa kila mwezi.
Mafao ya bima ya maisha Kifo au ulemavu wa Kudumu;
Mpango
wa kuwekeza kwa Awamu: Kinga ya bima ya maisha ina thamani sawa na
kiasi kisicholipwa na mwekezaji kwa muda uliosalia katika mpango wake wa
uwekezaji.
Mpango wa
Kuwekeza kwa Mkupuo: Kinga ya Bima ya Maisha ina thamani sawa na kiwango
alichochagua mwekezaji. (Muhimu: kiwango cha juu cha kulipwa ni Sh.
milioni 25).
Mafao ya
bima ya ajali: Mwekezaji atalipwa asilimia 20 ya kiwango kilichokusudiwa
katika mpango wa uwekezaji, hata hivyo kiwango cha juu ni Sh5 milioni
tu.
Mafao ya gharama za
mazishi: Kila mwekezaji atalipwa Sh.500, 000/= kwa ajili ya mazishi
endapo atafariki bila kujali kiwango alichowekeza.
Mkono
wa Pongezi: Mfuko utatoa mkono wa pongezi kwa mwekezaji ambaye
atakamilisha miaka kumi ya mpango wake wa uwekezaji au kama atafariki
ndani ya mwaka wa mwisho wa mpango wake wa uwekezaji.
MFUKO WA WATOTO
Mfuko
huu ni mpango uliowazi kwa watoto unaokusudia kukuza mtaji kwa muda
mrefu kupitia uwekezaji wa mseto kwa kuwekeza kwenye hisa
zilizoorodheshwa kwenye soko la hisa na dhamana.
Umriwa Mtoto wa Kujiunga na Mfuko: Uwekezaji unafanywa kwa jina la motto aliye chini ya miaka18.
Nani anaruhusiwa kuwekeza
Mfuko
uko wazi kwa watanzania walio ndani na nje ya nchi kama watubinafsi,
kampuni, taasisi, benki, asasi za kiraia. Uwekezajiufanywe kwa manufaa
ya mtoto.
Uwiano wa Rasilimali: Mfuko utawekeza
katika uwiano wa dhamana zenye mapato ya kudumu asilimia 0 hadi
asilimia 100 na hisa zilizoorodheshwa asilimia 0 hadi asilimia 50.
Chaguo
la mpango wa uwekezaji: Mfuko unatoa fursa za kukuza mtaji. kiwango cha
chini cha kuwekeza:(a) kiwango cha chini cha kuwekeza ni Sh.10,000 na
(b) kiwango cha chini cha uwekezaji wa nyongeza utakuwa Sh.5,000. Hata
hivyo hakuna kima cha juu cha kuwekeza.
Ukwasi:Uuzaji wa vipande vyote /sehemu ya vipande vilivyowekezwa unaruhusiwa pale mtoto mnufaika anapotimiza miaka 12.
Hata
hivyo uuzaji wa vipande vyote au baadhi unaweza kuruhusiwa pale
inapolazimu, mfano mahitaji ya fedha kwa ajili ya matibabu kwa ajili ya
mototo mnufaika au kwa ajili ya sababu nyingine ya msingi.
MFUKO WA JIKIMU
Madhumuni
Mfuko
huu ni mpango uliowazi wenye lengo la kukuza na kutoa gawio kutokana na
mapato ya ziada katika vipindi tofauti na pia kukuza mtaji kwa
mwekezaji wa muda mrefu.
Chaguo la mpango wa uwekezaji
Mfuko unatoa fursa mbili za uwekezaji-Mapato ya robo mwaka na mapato ya mwaka yaliyoambatanishwa na ukuaji wa vipande.
Nani
anaruhusiwa kuwekeza: Mfuko uko wazi kwa watanzania waliondani na nje
ya nchi, watu binafsi, kampuni / taasisi,mabenki, asasizakiraia (NGO)
kama inavyoonyeshwa kwenyewaraka huu.
Kiwango
cha chini cha kuwekeza: Ni Sh. milioni 2 kwa mpango wa mapato ya robo
mwaka na Sh milioni 1 kwa mpango wa gawio kwa mwaka na Sh. 5,000 kwa
mpango wa ukuaji wamtaji kwa mwaka.
Uwekezaji
wa nyongeza: Kiwango cha chini cha uwekezaji wa nyongeza/unaofuata ni
Sh 15,000 kwa mpango wowote wa gawio na Sh 5,000 kwampango wa ukuaji wa
mtaji kwa mwaka, hakuna ukomo wa kiwango cha kuwekeza.
Makato ya kodi: Kulingana na sheria za sasa, kodi ya mapato haitotozwa kwenye gawio litokanalo na uwekezaji kwenye mfuko huu.
Uhamishaji
wa Vipande: Uhamishaji wa vipande kutoka kwenye mfuko mmoja kwenda
mwingine kati ya mifuko inayoendeshwa na Dhamana ya Uwekezaji Tanzania
unaruhusiwa. Uhamishaji huu utatumia thamani halisi ya kipande kwa
wakati huo bila gharama yoyote.
Uhamishaji
huo utafanywa kwa mauzo ya vipande kutoka kwenye mfuko mmoja na
kuviwekeza kwa kununua vipande kwenye mfuko mwingine, ilimradi sifa za
kuwekeza kwenye mfuko mwingine zimezingatiwa.
MFUKO WA UKWASI
Madhumuni:
Mfuko huu ni mpango ulio wazi unaotoa njia nyingine ya uwekezaji kwa
wawekezaji wanaotaka kuweka fedha zao kwa kipindi cha muda mfupi na
katika kiwango kilichopo kwenye ushindani. Hatari/athari kidogo katika
uwekezaji na ukwasi wa hali ya juu ndio dhumuni hasa la mfuko huu.
Sera ya uwekezaji: Kiwango cha chini cha uwekezaji katika masoko ya fedha na dhamana zenye kutoa mapato ya kudumu 100%
Chaguo
la mpango wa uwekezaji: Mfuko huu unatoa fursa ya kukuza mtaji na
mwekezaji anaweza kujitoa katika Uwekezaji wakati wowote pasipo na
gharama.
Nani anaruhusiwa
kuwekeza: Mfuko uko wazi kwa mtanzania aliye ndani au nje ya nchi,
inahusisha watu binafsi (ikijumuisha watoto), na wawekezaji wasio watu
binafsi kama mifuko ya pensheni, benki/mashirika taasisi za serikali,
vyombo vya ulinzi na usalama, asasi zisizo za kiserikali na Mashirika
mengineyo n.k
Kiwango cha chini cha uwekezaji: a) Uwekezaji wa mwanzo= Shs 100,000 mauzo yanayofuata, Shs 10,000
Kiwango cha juu cha uwekezaji: Hakuna kiwango cha juu cha kuwekeza.
Umiliki
wa Vipande: Umiliki wa mtu mmoja na umiliki wa pamoja unaruhusiwa
katika mfuko huu. Hata hivyo, umiliki wa pamoja hauzihusu
taasisi/kampuni.
Ukwasi:
Baada ya kipindi cha utulivu kumalizika, uuzaji wa vipande utafanyika
kila siku ya kazi. UTT AMIS itatuma malipo ya mauzo ya vipande ndani ya
siku tatu za kazi baada ya kupokea fomu za maombi. Fedha za mauzo
zitatumwa moja kwa moja katika akaunti ya benki ya mwekezaji.
Tozo la kujiunga na kujitoa: Mwekezaji hatotozwa gharama yeyote ya kujiunga au kujitoa katika mfuko
Kigezo: Dhamana za Serikali za siku 35.
Ulinzi
wa mtaji: Lengo kuu ni kulinda mtawanyo wa uwekezaji ili kutoathiri
thamani ya vipande huku mtazamo mkuu ukiwa ni kipato cha uhakika.
MFUKO WA HATI FUNGANI
Huu
ni mfuko unaowekeza katika hati fungani za serikali, makampuni na
katika masoko ya fedha. Hivyo hutoa faida ya uhakika kulingana na hali
ya soko. Kiwango cha chini cha kuanza kuwekeza ni 50,000 kwa mpango wa
kukuza mtaji ,10,000,000 kwa mpango wa gawio kila mwezi na shilingi
5,000,000 kwa mpango wa gawio kila baada ya miezi sita. Nyongeza kwa
mipango yote mitatu shilingi 5000 au zaidi.
Kuwekeza kwa kutumia simu kwa kubonyeza namba *150*82#, Kufahamu zaidi tembelea www.uttamis.co.tz au piga bure; 00800112020.
No comments:
Post a Comment