Mwimbaji wa nyimbo za injili, Upendo Nkone akiimba moja ya
nyimbo zake wakati wa kuwatambulisha wanamuziki wataoshiriki tamasha la Pasaka
jijini Dar es Salaam. Katikati ni Mwenyekiti wa maandalizi ya
tamasha hilo, Alex Msama na kulia ni mwimbaji Bonny Mwaitege. (Picha na Habari Mseto Blog)
Mwimbaji wa nyimbo za injili, Bonny Mwaitege akiimba moja ya
nyimbo zake wakati wa kuwatambulisha wanamuziki wataoshiriki tamasha la Pasaka
jijini Dar es Salaam jana. Katikati ni Mwenyekiti wa maandalizi ya
tamasha hilo, Alex Msama.
Mwenyekiti wa maandalizi ya tamasha hilo, Alex Msama akizungumza na waandishi wa habari mara baada ya kuwatambulisha baadhi ya waimbaji watakaoshirika katika tamasha la Pasaka 2013.
Na Mwandishi Wetu
WAIMBAJI
Upendo Nkone na Boniface Mwaitege wamesema wamejipanga vilivyo kufikisha neno
la Mungu kwa kupitia karama ya uimbaji katika Tamasha la Pasaka litakalofanyika
Machi 31 kwenye Uwanja wa Taifa, jijini Dar es Salaam.
Nkone kwa
upande wake alisema juzi kuwa amekuwa kwenye maandalizi ya uhakika ili siku ya
tamasha hilo aweze kufanya vizuri kutowaangusha wapenzi na mashabiki
waliomwezesha kuteuliwa kupitia ujumbe mfupi wa maneno waliokuwa wanatuma kumpendekeza.
“Nimepata
furaha kwa waamini kutambua kazi yangu, ndio maana na najihisi nina deni, hivyo
nitajitahidi siku hiyo nyimba zangu zinazofahamika na mpya uitwao ‘Nimebaki na
Yesu’ ambao unachochea ibada kwa waamini,” alisema Nkone.
Nkone ametoa
wito kwa wapenzi, mashabiki na wadau kwa ujumla wa muziki wa injili kujitokeza
kwa wingi siku hiyo kwenye Uwanja wa Taifa ambapo mgeni rasmi atakuwa Waziri
Mkuu, Mizengo Pinda.
Naye
Boniface Mwaitege ameshukuru kupata nafasi ya kuimba kwenye tamasha hilo la
kimataifa ambalo safari hii litafanyika pia mkoani Dodoma, Mwanza, Iringa,
Mbeya na Mara, akiwasihi wapenzi na mashabiki wa muziki wa injili kujitokeza
kwa wingi.
“Mwaka jana
nilitamani kuimba pamoja na Rebecca Malope, bahati haikuwa yangu, nashukuru
safari hii nitaimba jukwaa moja na Sipho Makhabane wa Afrika Kusini, John Lissu, Upendo Kilahiro na
Rose Muhando, Nkone na wengineo,” alisema Mwaitege.
Aidha,
Mkurugenzi wa Msama Promotions inayoratibu tamasha hilo, Alex Msama alisema
siku ya Tamasha, kundi la
Gloria
Celebrations litazindua albamu yake ya ‘Kuweni Macho’ ambayo pia itauzwa Uwanjani
hapo.
Kuhusu
viingilio, viti vya VIP, itakuwa sh 50,000, Viti maalum sh 10,000, Viti vya kawaida sh 5,000 na watoto
shilingi 2000.
No comments:
Post a Comment