Mwenyekiti wa Mkutano wa dharura wa klabu ya Simba, Mohamed
Wande akifafanua jambo wakati wa mkutano uliofanyika katika ukumbi wa Starlight
jijini Dar es Salaam jana na kumg’oa madarakani aliyekuwa Mwenyekiti wa klabu
hiyo, Ismail Aden Rage. Kushoto ni Mjumbe wa Kamati ya Maandalizi ya Mkutanohuo, Bi. Chuma Suleiman ‘Hindu’ na Katibu wa Mkutano huo, Mohamrd said. (Picha
na Habari Mseto Blog)
Mzee wa Simba, Ally Mselemu akizungumza wakati wa mkutano huo.
Mwanachama wa Simba Saidi Mkumba cheche.
Mwanachama wa Simba, sofia lubuva akitoa nondo zake za kumtaka Rage kung'oka madarakani.
DAR ES SALAAM, Tanzania
ZAIDI ya wanachama
700 wa klabu ya Simba leo wameung'oa madarakani uongozi wa klabu hiyo chini
ya Mwenyekiti wake Ismail Rage, huku majukumu wakimkabidhi aliyekuwa Mwenyekiti
wa Kamati ya Usajili, Zacharia Hanspope.
Wanachama hao
walifikia maamuzi hayo, katika mkutano huo wa dharura uliofanyika ukumbi wa
Starlight jijini Dar es Salaam, baada ya wajumbe walioudhuria kupiga kura juu
ya kuwa na mashaka na uongozi uliopo madarakani.
Mara baada ya kupiga
kura hizo wanachama hao walipendekeza Hanspope kwa kushirikiana na Al Kharoos
‘Malikia wa Nyuki’ katika kamati ya muda ambayo itafanya kazi yake mpaka msimu
huu 2012/2013 utakapomalizika.
Mkutano huo,
ulioongozwa kwa amani na utulivu chini ya Mwenyekiti wake Mohamed Wande, ulitoa
fursa kwa wanachama kutoa maoni yao kabla ya kutoa maamuzi hayo kwa mujibu wa
ibara ya 16(g) inayowaruhusu wanachama kuunda kamati ya muda ambayo itaisimamia
Simba mpaka uchaguzi mkuu utakapofanyika mara baada ya kutokuwa na imani na
viongozi.
Baadhi ya wanachama
waliotoa maoni walipendekeza Rage abwage manyanga popote alipo na kudai kuwa
anaendesha timu kidikteta na kisiasa huku wakimshinikiza kuendelea na siasa ili
awaachie Simba yao, wao wenye mapenzi nayo.
Wanachama hao, Amina
Mkumba kadi namba (05226) alisema “Rage hatufai Simba, kwa udanganyifu ambao
ameufanya katika klabu yetu mpaka tunafungwa ni zamu yake na yeye kufungwa sasa
tumechoka, usajili wenyewe danganya toto tumemchoka,”alisema, Nae Salm Simba
(05864) alisema “Alisema wanachama tunatakiwa kuungana na kuwa kitu kimoja, na
hapa tumopendekeze kamati ambayo itachunguza matumizi ya pesa za Simba na
tukibaini udanganyifu Rage alipe,”alibainisha.
Mbali na hao nae
Mzee Abdallah Jahali kadi namba (58) alisema “Rage huko aliko ajing’oe mwenyewe
maana tumemchoka kila siku propaganda tu mara uwanja mara Okwi hata fedha zake
hatuzioni anatufanya watoto tumechoka jamani nadhani hata picha la Yondani na
Twite mnalikumbuka,”alisema.
Huku Ras Simba
(5757) alilitaka Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), na Chama cha Usajili hapa
nchini kulitazama suala hili kwa jicho la tatu na kudai kuwa viongozi wao
hawafuati katiba hata kidogo ambayo imetungwa kwa ajili ya kuiongoza Simba.
No comments:
Post a Comment