March 17, 2013

WAUMINI WA KANISA LA WAADVENTISTA WA SABATO TANZANIA WAADHIMISHA SIKU YA HUDUMA NA MATENDO YA HURUMA KWA JAMII

 Mtaalamu wa kutoa damu kutoka Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii, Mpango wa Damu Salama, Dk. Abdu Juma  akimtoa damu mmoja wa waumini wa Kanisa la Adventista Wasabato, John William ikiwa ni sehemu ya maadhimisho ya Siku ya Huduma na Matendo ya Huruma kwa Jamii Ulimwenguni. Sherehe hizo zilifanyika jijini Dar es Salaam mwishoni mwa wiki. (Picha Habari Mseto Blog)

Mtaalamu wa kutoa damu kutoka Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii, Mpango wa Damu Salama, Linus Kupuya akimtoa damu mmoja wa waumini wa Kanisa la Adventista Wasabato, Dolka Juma ikiwa ni sehemu ya maadhimisho ya Siku ya Huduma na Matendo ya Huruma kwa Jamii Ulimwenguni. Sherehe hizo zilifanyika jijini Dar es Salaam mwishoni wiki.

DAR ES SALAAM, Tanzania

WAUMINI wa Kanisa la Waadventista wa  Sabato Tanzania wameungana na waumini wenzao ulimwenguni kusherehekea siku ya huduma na matendo ya huruma kwa jamii ambayo yaliadhimishwa jijini Dar es Salaam mwishoni mwa wiki.

Akizungumza wakati wa maadhimisho hayo, Mkurugenzi wa Idara ya Vijana Jimbo la Mashariki mwa Tanzania Mchungaji, Emmanuel Sumwa alisema kanisa hilo lilipanga kuwa siku hiyo iwe siku ambayo waumini wake wakisaidiwa na idara  ya vijana kutoa huduma za kijamii kwa jamii inayowazunguka.

“Kwa kuzingatia umuhimu wa siku hii waumini wa kanisa duniani kote wametembelea maeneo mbali mbali kwa ajili ya kutoa misaada kwa wahitaji ikiwa ni pamoja na kuchangia damu katika benki ya Damu salama, kutembelea hospitali, kutoa misaada kwa wagonjwa, kutembelea vituo vya watoto yatima, kituo cha kijiji cha watuwasiojiweza Msimbazi center, mahabusu ya watoto upanga na magereza,” alisema.

Mchungaji Sunwa alitaja maeneo yaliyotembelewa kuwa ni Mwananyamala, Muhimbili, Amana,Temeke, Lugalo, Nevy, Parestina, Mbwenimission, Ocean Road, Vijibweni Kigamboni, Mabagala Zakiena, Tumbi Kibaha, Dar group na vituo vya watoto yatima Bunju,Ungindoni na mburahati.

Pia mchungaji huyo aliwataka Watanzania kuwa na moyo wa kujitolea pale panapohitajika hasa kwa watu wasiojiweza na watoto wanaoishi katika mazingira magumu.

No comments:

Post a Comment

Pages