March 17, 2013

Airtel yakabidhi vitabu vya Mil 12Tsh shule za sekondari mikoa ya kusini · Yatoa vitabu vya hisabati na sayansi kwa shule nne za sekondari mikoa ya Lindi na Mtwara


Airtel kwa kupitia mradi wa shule yetu mwishoni mwa wiki imekabithi vitabu vya hisabati na sayansi kwa shule za sekondari Namangale, Sino, Lukuledi, Namjota, Liondo and Kiangala zilizopo  mkoani  Lindi na Mtwara
Katika halfa fupi ya makabithiano yaliyofanyika katika shule ya sekondari ya Sino  Mtwara Afisa elimu na taaluma mkoa wa Mtwara bwana Rajabu Saidi alisema” tunafahamu changamoto mbalimbali zinazoikumba sekta ya elimu nchini ikiwemo upungufu wa vitabu, na tunashukuru Airtel kwa kuliona hilo na kuchangi vitabu katika shule hizi za sekondari, mbali na tatizo la vitabu tunalo tatizo linguine la uhaba wa walimu wa masomo ya sayansi na hawawezi kupatikana bila kupata maarifa ya sayansi kwa kupitia vitabu vitabu hivi tunavyovipokea leo. vitabu hivyo ni mkombozi mkubwa kwa elimu nahasa masomo ya sayansi ambayo yamekuwa na changamoto kubwa kutokana na ukosefu wa vitabu”.

Kwa upande wake Meneja mauzo wa Airtel kanda kusini Brighton Majwala alisema” shule zina changamoto kubwa ambapo uwiano kati ya wanafunzi na vitabu haulingani na mahitaji ya kasi ya elimu tarajiwa. msaada huo umetolewa ili kupunguza tatizo la uhaba wa vitabu kwenye shule nyingi hapa nchini na hasa vitabu vya masomo ya sayansi. Airtel tunaendelea kushirikiana na serikali chini ya wizara ya elimu katika kuhakikisha tunapunguza tatizo la uhaba wa vitabu mashule na kuboresha sekta ya elimu nchini.”

Akitoa shukurani mara baada ya kupokea msaada wa vitabu hivyo, Mwalimu wa Shule ya Sekondari ya Namangale ya mkoani Lindi, Joseph William ameshukuru kwa msaada huo na kuitaka kampuni hiyo kuendelea kusaidia zaidi katika upatikanaji wa maabara ili wanafunzi waweze kujifunza zaidi masomo yasayansi huku akiahinisha kuwa msaada wa huo wa vitabu hautapunguza upungufu wa vitabu shuleni hapo bali utainua kiwango cha taaluma katika shule yetu.

Aidha mmoja ya wanafunzi wa shuleni hapo alisema sisi wanafunzi tutavitunza vitabu hivi na kuvitumia vizuri ili kuinua taalama katika shule yetu na mikoa ya kusini kwa ujumla.

Airtel chini ya mpango wake wa shule yetu inaendelea kutimiza dhamira yake ya kuhakikisha kiwango cha elimu kinaongezeka, kwa kuchangia  nyenzo za kufindishia ikiwemo vitabu vya ada na kiada katika shule mbalimbali za sekondari nchini.

No comments:

Post a Comment

Pages