Na Mwandishi Wetu
ZAIDI ya walimu na wanafunzi 25,000 kutoka mikoa tisa nchini
wanatarajia kupata nafasi adhimu ya kujifunza kupitia mfumo wa digitali kwenye shule zao.
Hii inatokana na ushirikiano kati ya Airtel na British Council kutanua nafasi ya kunufaika na huduma inayotolewa na Airtel ya kuunganishiwa 5GB za internet kwa mwezi katika mpango wa miaka mitatu kwenye vituo 22 vya mfano wa matumizi ya digitali vilivyopo katika shule mbalimbali nchini.
Kampuni ya Airtel itaunganisha huduma ya internet kwenye vituo vyaBritish Council, shule hizo na jamii inayozizunguka.
Vituo hivyo vyadigitali tayari vimekwishaandaliwa kupitia ushirikiano na Microsoft huko Arusha, Bagamoyo, Kilimanjaro, Iringa, Mbeya, Ruvuma, Dodoma, Zanzibar na Mara.
Kasi ya ajabu ya upatikanaji wa internet kwenye maeneo hayo kutoka Airtel unawahakikishia walimu na wanafunzi fursa ya kupata elimu isiyo na kikomo.
Vituo hivyo kwenye shule zilizochaguliwa ni sawa na vituo vya TEKNOHAMA (ICT) kwa walimu, wanafunzi na wakazi wa maeneo husika.Kwa miaka mitatu iliyopita, mamia ya wanafunzi nchini wamenufaika na mpango wa British Council wa kuwaboreshea watoa elimu mchakato wa kujifunza na kufundisha kwa kupitia TEKNOHAMA.
Ni nia ya British Council kusapoti matumizi ya TEKNOHAMA katika shule za Afrika kuwa endelevu.
Akizungumza wakati wa hafla ya kuzinduliwa kwa ushirikiano huo,
Mkurugenzi Mtendaji wa Airtel, Bw. Mr. Sunil Colaso alisema:
"Airtel inaamini katika kuiwezesha jamii kupitia elimu, na leo
tunajivunia kupata nafasi ya kushirikiana na British Council katika
juhudi za kuikuza sekta ya elimu kupitia TEKNOHAMA," na kuongeza: "kutokana na kukua kwa sekta ya TEKNOHAM katika dunia ya kisasa, ni muhimu sana kuwapa ujuzi watoto wetu wakiwa katika umri mdogo. "Mkurugenzi wa British Council nchini, Bw. Richard Sunderland, alisema:
"Ushirikiano huu na Airtel unajenga na kuimarisha kile kinachojulikana kama 'Badiliko partnership' kati ya British Council na Microsoft, umoja unaolenga kusambazwa kwa TEKNOHAMA kwenye shule mbalimbali nchini," akaongeza: "ni ushirikiano utakaoboresha ubora wa maisha ya jamii kwa njia ya uwajabikaji wa makampuni kwa jamii (corporate social responsibility) kupitia elimu.
" British Council imewekeza katika ushirikishwaji wa kidigitali unaoziwezesha shule za Afrika kushirika katika ubadilishanaji wa maarifa na mawazo duniani.
TEKNOHAMA iliyoboreshwa huwawezesha walimu kuyaunganisha madarasa yao na mengine popote duniani, hivyo kuwapa wanafunzi kitu kipya kimataifa na kuwa na utambuzi mpana. Katika kuunga mkono juhudi za serikali kwenye eneo hilo, British Council imeandaa warsha maalumu ya kuzungumzia sera kwenye nchi mbalimbali kuizungumzia hilo, na hapa nchini warsha hiyo itafanyika mwezi ujaoBritish Council.
Mkurugenzi wa mawasiliano wa Airtel bi Beatrice Singano Mallya akiongea wakati wa uzinduzi wa ushirikiano kati ya kampuni ya Airtel na British council utakaowawezesha walimu na wanafunzi kupata nafasi adhimu ya kujifunza kupitia mfumo wa digitali kwenye shule zao. Mradi huo utashirikisha shule za sekondari katika mikoa mbalimbali nchini. Pichani kushoto ni Meneja huduma za jamii Hawa Bayumi , Kulia ni Mkurugenzi wa British Council Tanzania bwana Richard Sunderland leo.
Mkurugenzi wa British Council Tanzania bwana Richard Sunderland akiongea wakati wa uzinduzi wa ushirikiano kati ya kampuni ya Airtel na British council utakaowawezesha walimu na wanafunzi kupata nafasi adhimu ya kujifunza kupitia mfumo wa digitali kwenye shule zao. Mradi huo utashirikisha shule za sekondari katika mikoa mbalimbali nchini. Kushoto ni Mkurugenzi wa mawasiliano wa Airtel bi Beatrice Singano Mallya. Kulia ni Meneja Mradi British Council Tanzania, Bi Lilian Msuya
No comments:
Post a Comment