KAMPUNI za simu za mkononi zimemgomea
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kuhusu tozo la sh 1,000 kwa mwezi la
laini za simu (simu card) lililopitishwa na Bunge mwezi Julai mwaka huu.
Sheria hiyo inaendelea kuitafuna
serikali ya Chama Cha Mapinduzi (CCM), ambapo Mamlaka ya Mapato (TRA) kupitia
barua yake TRA/CLT/TELCS kwenda kwa kampuni hizo imeelekeza kuanza kutoza
kodi ya laini za simu kwa miezi mitatu tangu Julai hadi Septemba mwaka huu kwa
wananchi wote wanaomiliki laini za simu,
Barua hiyo inaelekeza kuwa: “Sheria
ya fedha ya mwaka 2013 ilianzisha kodi ya laini za simu na gharama za
kutuma na kupokea pesa, tarehe ya utekelezaji ilipaswa kuanza Julai 1, mwaka
huu… tumepitia kumbukumbu za makusanyo yetu kupitia sheria hiyo mpya ya
fedha ya mwaka 2013, tunasikitika kuwa malipo haya hayakufanyika, tunahitaji
malipo hayo yafanyike ndani ya siku 14.”
Barua hii ni kinyume kabisa cha kauli
iliyotolewa na Katibu wa Itikadi na Uenezi wa CCM, Nape Nnauye, kuwa serikali ni sikivu, lakini pia inaonesha
kampuni za simu zimemgomea Rais Kikwete kuhusu tozo hilo, ingawa TRA inaendelea na mkakati wa utekelezaji wa
sheria hiyo inayoamrisha kila mmiliki wa laini ya simu kulipia sh 1,000 kwa
mwezi.
Licha ya Rais Kikwete kufanya uamuzi
nje ya Bunge kuongea na wenye kampuni za simu, huku Nape akijigamba kuwa
serikali ya CCM ni sikivu na imesikia kilio cha wananchi, suala hilo
halijatatekelezwa.
Rais Kikwete
alikaririwa akiwaambia wadau hao wa mawasiliano kwamba: “Nakuombeni kaeni
pamoja, wekeni bongo zenu pamoja, wekeni akili zenu pamoja tutafute namna gani
tutajaza pengo hili la sh bilioni 178 endapo tutakubaliana kuwa kodi hii
inawabebesha wananchi mzigo mzito, na kuwa pengine menejimenti ya kodi yenyewe
ni ngumu.”
No comments:
Post a Comment