BARCELONA, Hispania
Kiungo Mjerumani, Mesut Ozil atakuwa akicheza pambano lake la kwanza la Mabingwa Ulaya akiwa na jezi za Gunners, iliyomsajili kwa dau la pauni milioni 42.4 akitokea Real Madrid ya Hispania
MABINGWA mara nne wa michuano ya mabingwa wa Ulaya, FC
Barcelona ya hapa, leo watakuwa dimba la Camp Nou kuwaalika Ajax Amsterdam ya
Uholanzi, ambayo pia imetwaa ubingwa huo mara nne, katika pambano la ufunguzi wa
‘Kundi la Kifo’ la H.
Barca walio chini ya kocha mpya, Gerardo ‘Tata’ Martino
aliyerithi mikoba ya Tito Vilanova, itakuwa na shughuli pevu katika mechi hiyo kukivaa
kikosi kinachonolewa na nyota wa zamani wa Barcelona na timu ya taifa ya
Uholanzi, Frank de Boer.
Tayari Tata Martino amejinasibu kushinda mechi ya nyumbani,
ingawa alikiri kuwa watalazimika kuwa makini na kutumia kila kosa la wapinzani
ili kufanikisha nia ya kuanza vema mchakamchaka huo utakaohitimishwa Mei
mwakani.
Pambano jingine la kundi H la michuano hii, linazikutanisha
AC Milan ya Italia na Celtic ya Uskochi, litakalopigwa kwenye dimba la San Siro
jijini Milan, ambalo wenyeji wataingia bila kiungo wake mpya Ricardo Kaka
aliyerejea hapo akitokea Real Madrid.
Kwingineko, jijini London, wenyeji wa dimba la Stamford
Bridge na mabingwa wa Europa League, Chelsea watakuwa nyumbani kuwaalika FC
Basle ya Uswisi, katika ufunguzi wa jaribio la klabu hiyo kutwaa taji la Ulaya
kama ilivyofanya mwaka jana.
Ikiwa chini ya kocha wake wa zamani Jose Mourinho aliyerejea
Darajani akitokea Real Madrid, Chelsea itaingia dimbani leo ikitoka kuugulia
maumivu ya kichapo katika pambano la Ligi Kuu ya England, ilikoangukia pua kwa
bao 1-0 dhidi ya Everton.
Chelsea inaikaribisha Basle ikijivunia uwapo wa mshambuaji
Mcameroon, Samuel Eto’o aliyeutua hapo akitokea Anzhi Makhachkhala ya Russia.
Katika mechi nyingine ya kundi hilo la E, Schalke 04 ya
Ujerumani, itaialika Steaua
Bucharest ya Romania kwenye dimba la Veltins Arena.
Katika kundi la F, Washika Bunduki wa jiji la London,
Arsenal watakuwa ugenini ndani ya dimba la Stade Velodrome jijini Marseille
kuwava wenyeji Olympique Marseille ya Ufaransa katika ufunguzi mwingine
unaosubiriwa kwa hamu.
Kiungo Mjerumani, Mesut Ozil atakuwa akicheza pambano lake
la kwanza la Mabingwa Ulaya akiwa na jezi za Gunners, iliyomsajili kwa dau la
pauni milioni 42.4 akitokea Real Madrid ya Hispania.
Wanafainali wa msimu uliopita, Borussia Dortmund ya
Ujerumani, watakuwa ugenini San Paolo jijini Naples, kuwavaa wenyeji Napoli
walio chini ya kocha Rafael Benitez na nyota kadhaa waliotua klabuni hapo
kiangazi hiki.
Katika ufunguzi wa kundi G, FK Austria Vienna watakuwa
nyumbani kwenye Uwanja wa Franz Horr kuwaalika FC Porto ya Ureno, huku Atletico
Madrid ya Hispania ikiumana na Zenit St Petersburg kwenye Uwanja wa Vicente
Calderon jijini Madrid.
RATIBA YA MECHI ZA LEO KWA UFUPI
KUNDI E
Schalke 04 v Steaua Veltins-Arena
Chelsea v FC Basel Stamford Bridge
KUNDI F
Marseille v Arsenal Stade Vélodrome
Napoli v Dortmund Stadio San Paolo
KUNDI G
Austria Wien v FC Porto Ernst-Happel
Atl. Madrid v Zenit Vicente
Calderón
KUNDI H
AC Milan v Celtic San Siro
Barcelona v Ajax Camp
Nou
Supersport.com/uefa.com
No comments:
Post a Comment