HABARI MSETO (HEADER)


Breaking

September 26, 2013

Sitaki CCM; Itufikishe mahali wananchi Wachague Kifo!

Na Bryceson Mathias
KATIKA Wosia wa Baba Mwl. JK Nyerere aliye Mwanzilishi wa Taifa hili kwa kuwa na Uhuru  alisema katika Kitabu chake cha Uhuru na Umoja (Freedom and Unity), “Ni rahisi mno kuliwasha taifa la watu waliokwazika”.
Taifa hili watu wamekwazika na mambo mengi kiasi ambacho unaweza kutibu majeraha yake makubwa ambayo yanalikabili taifa kwa kila mmoja analosema usiweze, maana kila mtu na eneo alipo  kazini, mashambani, katika biashara, maofisini, makanisani, ni majreha; Hivyo tusiwalaumu wapinzani.
Hivi sasa, wananchi wamekuwa wakikerwa na mambo mengi likiwemo tatizo la Ardhi, Mapigano ya Wakulima na Wafugaji, Watu kufanyiwa vitendo vya Unyama na uharamia wa Uteswaji, kumwagiwa Tindikali na kuvunjiwa Majumba.
Hali hiyo inawafanya wananchi wachoshwe na Serikali na wakati mwingi kufikia kuichukia bure Serikali yao, msingi mkubwa ukiwa ni kero za wazi na Dhuluma, Rushwa na Ufisadi uliokithiri miongoni mwa viongozi, huku chama tawala (CCM), aidha kinawakumbatia au hakiwaoni.
Uzembe wa viongozi kutowawajibisha hivyo, pia unakichafua CCM na kukipaka matope, pengine kutokana na watu wake kutowajibiki kikamilifu kwa wananchi, na pengine kutowakemea kwa mabaya wanayofanya mchana kweupe!
Ardhi ambayo watanzania kila siku wananyang’anywa na kupewa wageni tena nyakati zingine kwa kutumia mitutu na nguvu ya Dola bila kuthamini haki, ni moja ya mambo ambayo  CCM isipokuwa makini itawafikisha watu kufanya maamuzi magumu hata wakatamani kifo.
Migogoro  ya wakulima na wafugaji isiyoisha kiasi cha kuwafanya waingie kwenye njaa iliyokithiri na hata kufika mahali pa kupata ulemavu wa kudumu na kupoteza maisha yao, ni janaga linguine linalopaswa kuangaliwa kwa umakini ili kuliepuka.
Vitendo vya unyanyasaji vinavyofanywa na wawekezaji hasa wanaotoka nje dhidi ya wananchi wazawa, navyo ni tatizo linguine sugu ambalo lisipochukuliwa hatua mahususi za kulikomesha, baadaye litasababisha watu kukosa uvumilivu dhidi ya uonevu huo.
Ukitaka kumnyima mtu nidhamu basi mnyime Chakula na kumsababishia njaa. Njaa inaweza ikaamsha Hasira, na mtu akaamua kufanya lolote ili kinyamaziisha Njaa inayomsumbua, kwa sababu Njaa peke yake yenyewe inaua. Hivyo kabla ya kumuua mtu hufanya lolote kuizuia.
Mamuaji yasiyo na makemeo, yanayoendelea kutokea nchini huku damu za watu zikimwagika kana kwamba watu wanatoa kafara, zina machungu makubwa kwa familia zinazotendewa na hatimae watendaji hubaki wakiranda barabarani bila kuchukuliwa hatu zozote.
Migogoro mingi ya dhuluma katika maendeo ya kazi, ukiachia mbali ukosefu wa ajira kwa pamoja ni Bomu kubwa linalohifadhi mlipuko mkubwa, kwa sababu si jambo kawaida mtu adhulumiwe haki kwa kunyiwa mshahara wake wa mwezi hadi miezi minne wakati anafanya kazi.
Baadhi ya viongozi kwenye Vitongoji, Mitaa, Vijiji, Kata,Tarafa, Wilaya, Mikoa na Taifa wanaojifanya Miungu watu, Wenyeviti,Watendaji, Madiwani, Wabunge, Wakurugenzi, na Viongozi wa Kitaifa, nao ni Maudhi dhidi ya wananchi, nao wanaweza kusababisha Vilio.
Mchakato wa mapendekezo ya Katiba Mpya, nalo niwimbi lisipofanywa kwa kuzingatia Haki,  Ushirikishwaji wa kutosha hadi watu waridhike, ni Janga kubwa ambalo litaisababishia nchi uvunjifu wa Amani, watawala wasipokuwa makini.
Aidha dawa iliyobaki, ni viongozi wenye uchu wa kuendeleaa kukalia madaraka hata kama hawawezi, kuacha kufikiri wao wakidhani pekee ndio wanaweza, na badala yake wawashirikishe wananchi wote bila kujali itikadi, Dini,jinsia, Kabila,rangi na umri.
 nyeregete@yahoo.co.uk  0715933308

No comments:

Post a Comment

Pages