September 27, 2013

Waziri Simba: Watanzania wameathirika na Mangapi hujasema?
Na Bryceson Mathias
HIVI karibuni  nchini kumekuwa na madhara makubwa yaliyowapata wanawake, walemavu, wazee na watoto, lakini sijawahi kusikia waziri wa maendeleo ya jamii, Sophia Simba, akiyazungumzia isipokuwakauli za viongozi wakuu wa CHADEMA na CUF waliopinga Muswada wa Sheria ya Mabadiliko ya Katiba.
Akizungumza na wandishi hivi karibuni, Waziri Simba alikurupuka na kudai, kauli za Prof. Ibrahim Lipumba na Freeman Mbowe,  zililenga kuhatarisha amani, na kwamba, iwapo machafuko yakitokea waathirika ni wanawake, walemavu, wazee, Vijana na watoto.
Anaowataja Simba kuwa wataathirika, hivi karibuni wamekumbwa na Majanga Makubwa na ya kuhuzunisha, lakini sijawahi kusikia akikaripia wala kuwakemea wanaohusika tofauti na wajibu wake kama waziri husika na Mwenyekiti wa UWT anayeguswa na Majanga hayo.
Sikuwahi kumsikia Simba, akiwakoromea waliomuua kwa Bomu Mume wa Mjane Daudi Mwangosi, ambapo ndani mwake yumo Mama na Watoto wake waliohatarishwa na kuathirika kwa kukosa Amani ya kuwa na Baba yao, huku wakiishi kwa kuiogopa Dola.
Sijamsikia Simba, akitoa Kauli japo kulaani waliohusika na vifo vya kama ni Watoto, akina Mama, wazee, vijana au walemavu katika Mlipuko wa Bomu kanisani Z'bar,Arusha, na kwenye Mkutano wa Chadema. Kwamba hali hiyo inahatarisha Amani kwa wadau wake.
Si Arusha tu na Z'bar yalikotokea maafa ambayo yamewaathiri wadau wa Simba, bali karibu katika nchi nzima.
‘Mauaj ya Vikongwe, Walemavu, Wazee wenye Macho Mekundu, Mateso ya Wawekezaji wa Madini na Kemikali Nyamongo - North Mara, Melelan, ajali za barabarani na za Meli, bila kusahau Mafuriko ya Kilosa, Jangwani na Mabomu ya Ipagala na G/Mboto’.
Maafa na athari zote hizo, nakubaliana naye wahusika wakuu kwa sehemu kubwa ni wadau wa Simba kama anavyodai,  ambaye kama Mwenyekiti wa Jumuiya ya Umoja wa Wanawake wa Chama Cha Mapinduzi (UWT), alitakiwa kuwa na kauli za kuonya, kukemea, kulaanina kutoa Mwelekeo.
Mtu muongo, hasahau uongo wake, na mtu mkweli hawezi kusahau ukweli wake. Muongo hukumbuka kutetea uongo wake ili ajinufaishe kwa huo na mkweli husisitiza ukweli wake ili kulinda heshima na maisha ya wananchi.
Je, matamko ya Simba yana lengo la kulinda maisha ya watanzania au yana nia ya kulinda Uenyekiti wake wa UWT na nafasi yake na CCM kwa mgongo wa kuwataja na kuwatanguliza wadau wake? Kama ni kwa mustakabali wa maisha ya watu, mbona mengine hayakusemewa hivyo?
Achilia mbali hiyo ni mifano ya nyuma, lakini juzijuzi, mdau wake mtoto ambaye ameumwa kwa Miesi Sita akiwa anakunywa ‘Juice’ bila kuhudumiwa hadi ITV kupitia kwa Mtangazaji Mahiri Sam Mahela (apongezwe), alijitoa muhanga kumsemea apate msaada! Simba yupo wapi kwa Amani ya Mtoto huyo?
Kilichomsukuma Simba alisema ni “Septemba 21, mwaka huu, katika viwanja vya Jangwani, Mwenyekiti wa CHADEMA, Freeman Mbowe na Prof. Ibrahim Lipumba wa CUF walitoa kauli za uchochezi na zenye kuhatarisha amani ya Watanzania.
“Kauli ya Lipumba kuwa vijana wasikubali wakati wa kufanya mazoezi umefika na kauli ya Mbowe kuwa Oktoba 10 ni siku maalumu ya kitaifa ya ‘Civil Disobedience’, hizi ni kauli za kichochezi na Watanzania msikubaliane nazo,” alisema Simba.
Panya alikwenda kusali kanisani. Alipogeuka akamuona Paka amekaa. Panya; humu tumekuja kusali si kufukuzana! Paka; humu tunakula hadi mwili wa Yesu, seuse wewe?
nyeregete@yahoo.co.uk 07159333308

No comments:

Post a Comment

Pages