Rais wa Jamhuri ya
Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete amewasili mjini Iringa
jioni ya leo, Jumapili, Oktoba 13, 2013, kwa ziara ya siku mbili ya kikazi
mkoani Iringa. Rais Kikwete amefuatana na Mama Salma Kikwete.
Shughuli
kubwa ambazo Mheshimiwa Rais atazifanya wakati wa ziara hiyo ni kushiriki
Kumbukumbu ya Baba wa Taifa Mwalimu Julius Kambarage Nyerere, kuwa mgeni rasmi
katika Kilele cha Mbio za Mwenge Kitaifa mwaka huu wa 2013 na Kilele cha Wiki
ya Vijana.
Ndege iliyombeba
Rais Kikwete ilitua kwenye Uwanja wa Ndege wa Nduli mjini Iringa kiasi cha saa
12.20 jioni na kulakiwa na umati mkubwa wa wananchi wakiwemo wafuasi wa vyama
vya siasa vikiwamo CCM na Chadema.
Rais Jakaya Mrisho Kikwete akiwasili Uwanja wa Ndege wa Nduli mjini Iringa leo Oktoba 13, 2013 kuhudhuria Maadhimisho ya Kilele cha Mbio za Mwenye wa Uhuru, Wiki ya Vijana na Kumbukumbu ya Baba wa Taifa Mwalimu Julius Kambarage Nyerere zitaziofabyika kesho (Oktoba 14, 2013) katika uwanja wa Kumbukumbu ya Samora. PICHA NA IKULU.
Rais Jakaya Mrisho Kikwete akisalimiana na kamanda wa vijana Iringa Mhe Asas katika Uwanja wa Ndege wa Nduli mjini Iringa leo Oktoba 13, 2013 kuhudhuria Maadhimisho ya Kilele cha Mbio za Mwenye wa Uhuru, Wiki ya Vijana na Kumbukumbu ya Baba wa Taifa Mwalimu Julius Kambarage Nyerere zitaziofabyika kesho (Oktoba 14, 2013) katika uwanja wa Kumbukumbu ya Samora
Rais Jakaya Mrisho Kikwete akisalimiana na Mbunge wa Iringa mjini Mhe Msigwa katika Uwanja wa Ndege wa Nduli mjini Iringa leo Oktoba 13, 2013 kuhudhuria Maadhimisho ya Kilele cha Mbio za Mwenye wa Uhuru, Wiki ya Vijana na Kumbukumbu ya Baba wa Taifa Mwalimu Julius Kambarage Nyerere zitaziofabyika kesho (Oktoba 14, 2013) katika uwanja wa Kumbukumbu ya Samora.





No comments:
Post a Comment