Mkurugenzi Mtendaji wa Azam Media, Yusuph Bakhresa akibadilishana mawazo na wasanii.
Mkurugenzi Mtendaji wa Azam Media, Yusuph Bakhresa akizungumza na waandishi wa habari.
Salamu kwa wasanii.
Tunazindua.
Na Mwandishi Wetu
KAMPUNI ya Azam Media Ltd, imezindua Ofisi za Makao Makuu na kituo cha televisheni cha Azam, ambacho kitaanza rasmi kurusha matangazo ya moja kwa moja ya mechi za soka katika michuano ya Kombe la Mapinduzi 2013 visiwazi Zanzibar.
KAMPUNI ya Azam Media Ltd, imezindua Ofisi za Makao Makuu na kituo cha televisheni cha Azam, ambacho kitaanza rasmi kurusha matangazo ya moja kwa moja ya mechi za soka katika michuano ya Kombe la Mapinduzi 2013 visiwazi Zanzibar.
Akizungumza katika uzinduzi huo, Mkurugenzi Mtendaji wa Azam
Media, Yusuph Bakhresa, alisema kuwa ujio wa ofisi hizo unatoa fursa ya wateja
wao kupata uhakika wa mahali pa kuhudumiwa, huku akiwataka kuipokea Azam Tv
iliyosheheni kila kitu.
Alisema wadau wa soka Tanzania wataanza kushuhudia uhondo wa
matangazazo ya ‘live’ kuanzia katika michuano ya Kombe la Mapinduzi,
inayotarajia kuanza kutimua vumbi mwishoni mwa mwaka hadi Januari 12 ambayo
nilele cha Sikukuu ya Mapinduzi.
Bakhresa alisema kuwa, ubora wa huduma kupitia Chaneli 52
zinazopatikana katika king’amuzi cha Azam unawapa uhakika wa kutamba katika
tasnia ya habari, kupitia vipindi bora na bei nafuu za malipo ya kila mwezi,
ambavyo anaamini vitavutia wadau.
Alibainisha kuwa, kupitia chaneli mbili za Azam One na Two,
wapenzi wa soka nchini wataona ‘live’ matangazo ya Kombe la Mapinduzi kutoka
kwenye Uwanja wa Gombani, Pemba, ambao pia utakuwa ukishuhudia pia mechi za
kwanza kutanmgazwa ‘live.’
Michuano ya Mapinduzi 2013 itashirikisha klabu za Tanzania
Bara za Yanga, Azam FC, Mbeya City na Simba, ambazo zitachuana na zile za Pemba
Kombaini, Unguja Kombaini, KMKM na nyingine ambayo haijatambulishwa, pamoja na
Tusker ya Kenya.
Bakhresa alibainisha kuwa, baada ya kumalizika kwa Kombe la
Mapinduzi, Azam Tv itahamia katika mzunguko wa pili wa Ligi Kuu ya Vodacom,
kote huko wakitarajia kufanya vema kupitia mitambo bora na ya kisasa kuhimili
ushindani sokoni.
Aliongeza kuwa, Azam Media itambua ugumu wa tasnia ya habari
na ushindani uliopo, lakini wamejipanga na kwamba wana uhakika mitambo yao bora
ya kurushia matangazo itawewezesha kukabiliana na yote na hatimaye kuzishinda
kampuni kongwe nchini.
No comments:
Post a Comment