Na Ibrahim Yassin, Kyela
KATIBU mkuu wa
Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) Dkt,Wilbrod Slaa alisema kama chama
chake hakitasimamia misingi ya utawala bora haina sababu ya wananchi kuichagua
kuongoza nchi katika uchaguzi ujao wa mwaka 2015.
Kauli hiyo
aliitoa jana wakati akihutubia maelfu ya wananchi katika mkutano wa hadhara
uliofanyika katika uwanja wa Siasa wilayani Kyela mkoani Mbeya katika
muendelezo wa Opereshen Pamoja Daima ya M4c.
Dkt, Slaa
alisema kuwa watanzania wamefikishwa mahali pabaya na Serikali ya Chama Cha
Mapinduzi hali iliyopelekea Nchi ya Tanzania kuwa ya pili kwa umasikini katika
Nchi za Afrika wakati Nchi ni ya pili kuwa na rasilimali nyingi katika Afrika.
Alisema
kinachasababisha nchi kuwa masikini ni kutokana na misingi mibovu ya Serikali
ya Chama Cha Mapinduzi na kwamba ili nchi iondokane na hali hiyo wananchi
wanatakiwa kufanya maamuzi magumu ya kutoichagua tena katika uchaguzi ujao na
kuwa wanatakiwa kuichagua Chadema kuanzia vijiji hadi urais.
Alisema misingi
mibovu ya Chama cha mapinduzi ndiyo sababu ya nchi hii kuyumba na kupelekea
hadi kuwa wapili kutoka mwisho kwa umasikini Afrika hali ya kuwa Tanzania ni ya
pili kuwa na lasilimali nyigi inayoweza ikawaondoa katika lindi la umaskini
kama viongozi wangekuwa na mipango mizuri isiyokuwa ya kifisadi.
No comments:
Post a Comment