Rais wa taasisi ya isiyo ya kiserikali ya ISACA Tanzania, Boniface Kanemba akifungua semina kuhusu usalama wa fedha kwenye mitandao ya simu pamoja na mkutano mkuu wa taasisi hiyo uliofanyika Dar es Salaam.
Wadau.
Mshiriki wa semina hiyo akiuliza swali.
Washiriki wa semina.
Baadhi ya washiriki wa semina hiyo.
Ofisa wa PPF akitoa mada.
Ofisa Mtendaji Mkuu wa wakala wa Serikali Mtandao ambaye pia ni Makamu wa Rais wa taasisi ya isiyo ya kiserikali ya ISACA Tanzania, Dk. Jabir Bakari Kuwe (kulia), akitoa mada wakati wa mkutano wa wadau, kuhusu usalama wa fedha kwenye mitandao ya simu pamoja na mkutano mkuu wa taasisi hiyo uliofanyika Dar es Salaam.
Dk. Carina Wangwe akitoa mada.
Rais wa taasisi ya isiyo ya kiserikali ya ISACA Tanzania, Boniface Kanemba (kulia) akifafanua jambo wakati wa mkutano wa wadau, kuhusu usalama wa fedha kwenye mitandao ya simu pamoja na mkutano m.kuu wa taasisi hiyo uliofanyika Dar es Salaam.
Mmoja wa washiriki wa semina hiyo akitoa mada.
Rais wa taasisi ya isiyo ya kiserikali ya ISACA Tanzania, Boniface Kanemba akizungumza na waandishi wa habari.
DAR ES SALAAM, Tanzania
DAR ES SALAAM, Tanzania
WANANCHI wametakiwa kuepuka kugawa taarifa zao muhimu kuhusiana na mawasiliano yao ya simu pamoja na taarifa muhimu za kibenki.
Tahadhari hiyo imetolewa kufuatia ongezeko la wizi wa fedha katika akaunti za benki na simu za mkononi unaofanywa na matapeli hapa nchini.
Rais wa Taasisi inayojishugulisha na Ukaguzi wa Mitandao ya ISACA Tanzania , Boniface Kanemba alisema kuwa matapeli hao wanaweza kutumia nambari za simu za mkononi na akaunti ya benki kujua namba za siri za kuchukulia fedha.
Alisema kuwa ili kuepuka wizi wa aina hiyo ni vema wananchi wakachukua tahadhari dhidi ya utoaji wa taarifa kwa kuwa inakuw ani vigumu kuwakamata pindi wakishafanya uhalifu huo.
Alisema kuwa matapeli wa aina hiyo walikuwa zaidi katika Kenya na lakini kwa sasa inaonekana wamevamia zaidi hapa nchini na kutumia ujuzi huo.
Alisema kuwa kwa ukanda wa Afrika Mashariki peke yake kiasi cha zaidi ya trilioni 80 zimeibwa kwa njia ya utapeli.
Aliongeza kuwa ili kukabiliana na hali hiyo tayari taasisi yake inaendelea na utoaji wa semina mbalimbali kwa wadau wa teknolojia ya mawasiliano na watu wa usalama kwa ujumla.
"Najau wizi wa aina hii ulikuwa zaidi katika nchi za Ulaya na Afrika Magharibi na ukanda huu wa Afrika ya Mashariki ulikuwa zaidi Kenya lakini kwa sasa hawa matapeli wamevamia ukanda huu wa Afrika Mashariki na hali inazidi kuwa mbaya"alisema Kanemba.
Taasisi hiyo ya ISACA ilianza kazi hapa nchini mwaka 2003 na imekuwa ikifanya ukaguzi wa usalama wa fedha na matukio mengine muhimu kwa njia ya mtandao.
No comments:
Post a Comment