January 08, 2014

MKUTANO MKUU WA WAFANYABIASHARA KUFANYIKA JIJINI DAR
MKUTANO Mkuu wa kujadili changamoto mbalimbali zinazowakabili wafanyabiashara ikiwemo mfumo mbaya wa uendeshaji  biashara nchini, unafanyika jijini Dar es Salaam Januari 9.

Katibu wa Umoja wa Wafanyabiashara Kariakoo, Sued Chemchem, alisema mkutano huo utawakutanisha viongozi wa wafanyabiashara kutoka mikoa yote ya Jamhuri ya Muungano, ambako unatarajiwa kuanza saa tatu asubuhu kwenye Ukumbi wa Diamond Jubilee jijini.

Alisema mkutano huo utajikita zaidi kujadili na kuandaa utaratibu ambao utaleta tija kwa ajili ya wafanyabiashara hao nchini.

Chemchem alisema  miongoni mwa mambo yatakayojadiliwa leo ni pamoja na uchaguzi wa wajumbe ambao wataunda tume yao kwa ajili ya kukutana na wataalam wa Wizara ya Fedha, Biashara na Viwana na wale wa TRA.

Alisema lengo la kukutana na wataalamu hao ni kutaka kutafuta ufumbuzi wa changamoto mbalimbali zinazojitokeza hususan matumizi ya mashine ya kutolea stakabadhi (EFD).

‘Tunatarajia mgeni rasmi atakuwa Waziri wa Viwanda na Biashara Abdallah Kigoda kama tulivyomuomba.  

“Huu ni mkutano muhimu na ndio mana tunawataka wafanyabiashara wote wafike, hakuna atakayefunga duka kwani kila duka linazaidi ya watu wawili, kwa wale wasio kuwa na wasaidizi watapima wenye umuhimu wa mkutano huo;”alisema Chemchem.

Hata hivyo baadhi ya wakazi wa jiji la Dar es Salaam wameingiwa na hofu kuwa huenda wafanyabiashara hao wasifungue maduka kwa ajili ya mkutano huo waliouita muhimu kuliko mambo yote.

No comments:

Post a Comment

Pages