January 31, 2014

MWILI WA SHEIKH WA MKOA WA MARA ULIPOWASILI UWANJA WA NDEGE MUSOMA
 Ndege iliyobeba mwili wa Marehemu, Sheikh Athuman Magee.
 Mkuu wa Mkoa wa Mara John Tupa akielekea kwenye Ndege kuongoza waombolezaji.  
Waombolezaji wakisubiri mwili kushushwa.
  Gari la JWTZ likiwa tayari kwa ajili ya kubeba mwili wa Sheikh wa Mkoa wa Mara, Athumani Magee aliyefariki dunia usiku wa Januari 28. 
  Waumini wa dini ya kiislamu pamoja na wananchi wa mji wa Musoma wakiwa Uwanja wa Ndege.
  Afidh Waziri mmoja wa watu waliotoka na Wmwili wa sheikh  Magee Dar akiangaliana rubani wa ndege.
Waombolezaji.
Mwili ukipelekwa nyumbani.

 Msafara wa mwili wa Sheikh magee ukielekea nyumbani kwake.
Msagara wa pikipiki ukisindikiza.
 Mkuu wa Mkoa wa Mara, akiwasili nyumbani kwa Sheikh Magee.
 Mwili ukishushwa.
  Baadhi ya waombolezaji.

MARA, Tanzania
MKUU wa mkoa wa Mara Mheshimiwa John Gabriel Tuppa ameongoza maelfu ya Wananchi wa Mji wa Musoma kupokea mwili wa Shekh wa Mkoa wa Mara Athumani Magee aliyefariki dunia usiku wa januari 28 katika hospitali ya Taifa Muhimbili alipokuwa akipatiwa matibabu.



Shekh Athumani Magee alifikwa na mauti baada ya kugua kwa muda na mrefu na kupatiwa matibabu katika hospitali ya rufaa Bugando kwa muda kabla ya kuhamishiwa Muhimbili kwa uangalizi zaidi na akiwa njiani kupelekwa nchini India kwa matibabu zaidi.

Baadhi ya waumini wa dini ya Kiislam waliokuwepo kwenye uwanja wa ndege Musoma wakiusubili mwili wa shekh Magee wamesema  wamepata pigo kubwa kutokana na msiba huo kutokana na Shekh kuwa mstari wa mbele katika kuhimiza masuala ya dini.

Shekh wa mkoa wa Mara anatarajiwa kuzikwa kesho kabla ya swala ya adhuhur katika makabari ya Musoma Bus mjini Musoma.

PICHA/HABARI KWA HISANI YA SHOMARI BINDA
   INNAH LILLAH WAINNAH ILLAH RAJIUUN


No comments:

Post a Comment

Pages