January 16, 2014

RAIS KIKWETE AWAONGOZA WAOMBOLEZAJI MSIBA WA JAJI GEORGE LIUNDI
 Rais Jakaya Kikwete, akitoa heshima za mwisho mbele ya jeneza lenye mwili wa marehemu, Jaji George Liundi wakati wa shughuli za kuagwa mwili huo zilizofanyika kwenye viwanja vya Karimjee jijini Dar es Salaam leo.
 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, na Makamu wa kwanza wa Rais wa Zanzibar, Maalim Seif, wakitoa heshima za miwsho mbele ya Jeneza lenye mwili wa marehemu Jaji George Liundi, wakati wa shughuli za kuagwa mwili huo zilizofanyika kwenye viwanja vya Karimjee jijini Dar es Salaam, leo. Kulia ni Rais Mstaafu wa awamu ya tatu Benjamin Mkapa, akielekea kutoa heshim za mwisho. 
 Rais Jakaya Kikwete (wa pili kushoto) Makamu wake Dkt. Mohammed Gharib Bilal, Makamu wa kwanza wa Rais wa Zanzibar, Maalim Seif, Mwenyekiti wa Tume ya Mabadiliko ya Katiba mpya, Jaji Joseph Warioba, Makamu mwenyekiti wa CCM Bara, Philp Mangula na Waziri wa Nchi-Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera na Uratibu na Bunge) William Lukuvi, wakishiriki Misa maalum ya kumuombea marehemu Jaji George Liundi, wakati wa shughuli za kuagwa mwili zilizofanyika kwenye viwanja vya Karimjee jijini Dar es Salaam leo. 
 Rais Jakaya Kikwete (wa pili kushoto) Makamu wake Dkt. Mohammed Gharib Bilal, Makamu wa kwanza wa Rais wa Zanzibar, Maalim Seif, na Waziri wa Nchi-Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera na Uratibu na Bunge) William Lukuvi (kushoto) wakijumuika na waombolezaji  katika misa maalum ya kumuombea marehemu Jaji George Liundi, wakati wa shughuli za kuagwa mwili zilizofanyika kwenye viwanja vya Karimjee jijini Dar es Salaam leo.
Rais Jakaya Kikwete (wa pili kushoto) Makamu wake Dkt. Mohammed Gharib Bilal, Makamu wa kwanza wa Rais wa Zanzibar, Maalim Seif, na Waziri wa Nchi-Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera na Uratibu na Bunge) William Lukuvi (kushoto) wakitafakari msiba huo wakati wa shughuli za kuagwa mwili zilizofanyika kwenye viwanja vya Karimjee jijini Dar es Salaam leo. 
 Sehemu ya wanafamilia wakishiriki shughuli hiyo.
 Sehemu ya wanafamilia wakishiriki shughuli hiyo.
 Mjukuu wa marehemu, ambaye ni mototo wa mtangazaji, Taji Liundi, akisoma wasifu wa marehemu.
 Baadhi ya viongozi wakielekea kutoa heshima za mwisho.
 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akiagana na Mmwenyekiti wa Chama cha CUF, Prof Ibrahim Lipumba, baada ya shughuli za kuagwa mwili wa marehemu Jaji George Liundi, zilizofanyika kwenye viwanja vya Karimjee jijini Dar es Salaam, leo.
Rais Jakaya Kikwete, akiagana na Makamuwa kwanza wa Rais wa Zanzibar, Maalim Seif, baada ya shughuli za kuagwa mwili wa marehemu Jaji George Liundi, zilizofanyika kwenye viwanja vya Karimjee jijini Dar es Salaam, leo.

No comments:

Post a Comment

Pages