Rais Jakaya Kikwete
akimkaribisha ikulu jijini Dar es Salaam, Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya
CRDB, Dk. Charles Kimei, (kushoto), alipofika kutoa msaada wa sh. milioni 100 kwa ajili ya kusaidia wahanga wa mafuriko yaliyozikumba wilaya tatu za Kilosa, Mvomero na Gairo katika Mkoa wa Morogoro, mwezi uliopita. Dk. Kimei alifuatana na baadhi ya viongozi wa benki hiyo.
Naibu Mkurugenzi Mtendaji Huduma Shirikishi wa Benki ya CRDB, Esther Kitoka (kushoto), akisalimiana na Rais Jakaya Kikwete ikulu jijini Dar es Salaam. Katikati ni Mkurugenzi Mtendaji wa CRDB, Dk. Charles Kimei.
Rais Jakaya Kikwete akisalimiana na Mkurugenzi wa Masoko Utafiti na Huduma kwa Wateja wa Benki ya CRDB, Tully Mwambapa.ikulu jijini Dar es Salaam. Katikati ni Naibu Mkurugenzi Mtendaji Huduma Shirikishi wa Benki ya CRDB, Esther Kitoka.
Mkurugenzi Mtendaji wa Bernki ya CRDB, Dk. Charles Kimei (kulia), Naibu Mkurugenzi Mtendaji Huduma Shirikishi wa Benki ya CRDB, Esther Kitoka na Mkurugenzi wa Masoko Utafiti na Huduma kwa Wateja wa Benki ya CRDB, Tully Mwambapa, wakimsikiliza Rais Jakaya Kikwete (hayupo pichani), ikulu jijini Dar es Salaam.,
Dk. Kimei akifafanua jambo kwa Rais Jakaya Kikwete.
Mazungumzo yakiendelea.
Dk. Charles Kimei akitoa maelezo mafupi kabla ya kukabidhi hundi ya Sh, milioni 100 kwa ajili ya wahanga wa mafuriko yaliyotokea mkoani Morogoro.
Rais Jakaya Kikwete
akipokea hundi ya sh. milioni 100 kutoka kwa Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya
CRDB, Dk. Charles Kimei (kushoto), kwa ajili ya kusaidia watu waliopatwa na
mafuriko Mkoani Mororo hivi karibuni.
Rais Jakaya Kikwete akiangalia kwa makini hundi aliyokabidhiwa.
Rais Jakaya Kikwete akiiweka katika bahasha hundi ya Sh, milioni 100 baada ya kupokea kutoka kwa Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya CRDB, Dk. Charles Kimei (kushoto), huku makini hundi aliyokabidhiwa, Naibu Mkurugenzi Mtendaji Huduma Shirikishi wa Benki ya CRDB, Esther Kitoka
Rais Dk. Jakaya Kikwete akimkabidhi hundi aliyokabidhiwa na uongozi wa Benki ya CRDB kwa Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu Sera, Uratibu na Bunge, William Lukuvi anayeshughulikia pia masuala ya maafa, William Lukuvi.
Rais Jakaya Kikwete (kushoto), akiwa katika picha ya pamoja na Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya CRDB, Dk. Charles Kimei.
Naibu Mkurugenzi Mtendaji Huduma Shirikishi wa Benki ya CRDB, Esther Kitoka akiwa katika picha ya pamoja na Rais Jakaya Kikwete.
Rais Jakaya Kikwete (kushoto), akiwa na Mkurugenzi wa Idara ya Njia Mbadala za Kibenki katika Benki ya CRDB, Joseph Witts.
Meneja Uhusiano wa Benki ya CRDB, Godwin Semunyu (kulia), akiwa na Rais Jakaya Kikwete.
Rais Jakaya Kikwete akiwa katika picha ya pamoja na Katibu wa Benki ya CRDB, John Lugambo.
Rais Dk. Jakaya Kikwete akiwa katika picha ya pamoja na uongozi wa Benki ya CRDB, Kushoto ni Katibu wa Benki ya CRDB, John Lugambo, Mkurugenzi wa Masoko Utafiti na Huduma kwa Wateja wa Benki ya CRDB, Tully Mwambapa, Mkurugenzi Mtendaji wa CRDB, Dk. Charles Kimei, Naibu Mkurugenzi Mtendaji Huduma Shirikishi wa Benki ya CRDB, Esther Kitoka, Mkurugenzi wa Idara ya Njia Mbadala za Kibenki,
Joseph Witts na Meneja Uhusiano wa Benki ya CRDB, Godwin Semunyu.
Rais Jakaya Kikwete (katikati), akiwa katika picha ya pamoja na viongozi wa Benki ya CRDB mara baada ya kupokea hundi ya sh. milioni 100 kutoka kwa Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya CRDB, Dk. Charles Kimei (wa pili kushoto), kwa ajili ya kusaidia watu waliopatwa na mafuriko Mkoani Mororo hivi karibuni. Kushoto ni Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu Sera, Uratibu na Bunge, William Lukuvi, Naibu Mkurugenzi Mtendaji Huduma Shirikishi wa Benki ya CRDB, Esther Kitoka (wa pili kulia), na Mkurugenzi wa Masoko Utafiti na Huduma kwa Wateja wa Benki ya CRDB, Tully Mwambapa.
Rais Dk Jakaya Mrisho Kikwete akimshukuru Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya CRDB, Dkt. Charles Kimei, baada ya kukabidhiwa hundi ya shilingi milioni 100 kutoka benki hiyo kusaidia waathirika wa mafuriko yaliyozikumba wilaya tatu za Kilosa, Mvomero na Gairo katika Mkoa wa Morogoro.
THE
UNITED REPUBLIC OF TANZANIA
DIRECTORATE
OF PRESIDENTIAL COMMUNICATIONS
Telephone: 255-22-2114512,
2116898
E-mail: ikulumawasiliano@yahoo.com
Fax: 255-22-2113425
|
PRESIDENT’S
OFFICE,
THE STATE HOUSE,
P.O.
BOX 9120,
DAR
ES SALAAM.
Tanzania.
|
Rais
wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete leo,
Jumanne, Februari 4, 2014, amepokea hundi ya Sh. milioni 100 kutoka Benki ya
CRDB kusaidia wahanga wa mafuriko yaliyozikumba wilaya tatu za Kilosa, Mvomero
na Gairo katika Mkoa wa Morogoro, mwezi uliopita.
Rais
Kikwete amekabidhiwa hundi hiyo na Mkurugenzi Mtendaji wa CRDB, Dk. Charles
Kimei katika shughuli fupi iliyofanyika Ikulu, Dar Es Salaam, na kuhudhuriwa
pia na Mhesimiwa William Lukuvi, Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu
anayeshughulikia pia masuala ya maafa.
Akizungumza
kabla ya kukabidhi hundi hiyo kwa Rais Kikwete, Dkt. Kimei amesema kuwa fedha
hizo ni sehemu ya Sh. Milioni 850 ambayo ni asilimia moja ya faida ya Benki
hiyo ambayo hutengwa kila mwaka kwa ajili ya kuunga mkono shughuli za jamii.
“Sote
tumeona madhara makubwa yaliyosababishwa na mafuriko haya. Watu wengine
wamepata hasara – akinamama, watoto, wajawazito na wazee. Hawa wote wanahitaji
misaada ya ziada ili kukabiliana na athari za mafuriko hayo,”
amesema Dkt. Kimei.
Akizungumza
kabla ya kupokea hundi hiyo, Rais Kikwete ameelezea kwa ufupi mafuriko hayo
yaliyotokea alfajiri ya Januari 22, mwaka huu, 2014 na athari ambazo zimetokana
na mafuriko hiyo katika maeneo ya Magole, Dakawa na Mateteni huko Dumila, Wilaya
ya Mvomero, ambayo aliyatembelea mwishoni mwa mwezi uliopita kujionea madhara.
“Waswahili
husema kuwa ajali haina kinga na ni kweli. Unajua mafuriko yaliyotokea katika
eneo la Dumila hayakutokana na wala na mvua ya pale. Mvua ilinyesha kule
Kiteto, Mkoa wa Manyara, lakini walioathirika kwa mafuriko ni hawa jamaa zetu
wa Dumila. Bahati tu ni kwamba mafuriko hayo yalilikumba eneo hilo alfajiri
wakati watu tayari wameamka na ndio maana hakuna mtu aliyepoteza maisha yake
katika eneo hilo,” amesema Rais Kikwete na
kuongeza:
“Watu
wamepata hasara kubwa. Baadhi nyumba zao zimesombwa na kuzolewa na maji,
nyingine zimebomoka, watu wamepoteza mali zao nyingi kama vile nguo na wengine
hata chakula chao kimesombwa na maji. Wanahitaji msaada na kwa kweli sisi
katika Serikali tunaishukuru sana CRDB kwa kutoa msaada huu kwa sabababu unachangia
katika jitihada za Serikali kukabiliana na tatizo hili.”
Akizungumza
katika shughuli hiyo, Mheshimiwa Lukuvi amesema kuwa tathmini mpya imeonyesha
kuwa watu walioathirika katika mafuriko
hayo ni 9,268 na kati ya watu hao kaya 522 hazina makazi kabisa baada ya nyumba
zao kubomolewa na maji, nyingi zaidi 466, zikiwa katika Wilaya ya Kilosa.
Amesema
kuwa nyumba 537 zimeharibika hata kama wenye nyumba hizo bado wanaendelea
kuishi ndani ya nyumba hizo na nyingine 1,036 ziliingiwa na maji hata kama
hazikuharibika.
Imetolewa
na:
Kurugenzi ya
Mawasiliano ya Rais,
Ikulu,
DAR
ES SALAAM.
04 Februari, 2014
No comments:
Post a Comment