Mkurugenzi wa Operesheni na Mafunzo wa Chadema, Benson Kigaila akizungumza na wajumbe wa mkutano wa Halmashauri kuu ya Chadema jimbo la Kalenga jana huku akionyesha katiba ya Chadema kabla ya wajumbe wa mkutano huo kupiga kura kumchagua mgombea ubunge jimbo hilo kupitia Chadema. (Picha na Francis Godwin)
Wajumbe wa mkutano wa kura za maoni Chadema jimbo la Kalenga wakiwa katika ukumbi wa St Dominic.
Francis Godwin na Denis Mlowe Iringa
WAKATI jana wajumbe wa Halmashauri kuu ya chama cha Demokrsia na maendeleo (CHADEMA) jimbo la Kalenga wameshiriki katika zoezi la upigaji wa kura za maoni kuchagua mmoja kati ya wanachama 13 waliojitokeza kurejesha fomu za kuomba kuteuliwa kuwa wagombea wa nafasi ya ubunge jimbo la kalenga kupitia chama hicho ,mkurugenzi wa Operesheni na Mafunzo wa Chadema, Benson Kigaila amesema chama chake kamwe hakitasimamisha mgombea dhaifu katika kinyang'anyiro hicho na lazima CCM kianze kuzoea kushindwa .
Huku mbunge wa viti maalum mkoa wa Iringa na mjumbe wa kamati kuu ya Chadema Bi Chiku Abwao akiwataka wana Kalenga kujenga imani na Chadema na kuwa haitakuwa tayari kumweka ndugu katika chaguzi hizo na kuwa CCM imeonyesha kuwadharau wana Kalenga kwa kuendekeza siasa za familia katika jimbo hilo jambo ambalo halikubaliki.
Akifungua mkutano huo wa kura za maoni katika ukumbi wa St Dominic mjini Iringa Kigaila alisema kuwa lengo la mkutano huo ni kuanzisha mchakato wa kumpata mgombea wa Chadema na kuwa Chadema ina matumaini makubwa ya kushinda katika jimbo hilo.
" CCM walikuwa wakisikilizia ni nani ambae Chadema itamsimamisha katika jimbo hilo na kuwa walidhani wapo peke yao ila sasa Chadema inatangaza rasmi kuwa mchakato wa kumpata mgombea wake umeanza na ni lazima apatikane mgombea ambae atakuwa ni tofauti na mgombea wa CCM....lazima CCM kwa hapa kilipofika kianze kuzoea kushindwa katika uchaguzi"
Alisema kuwa utaratibu wa kumpata mgombea wa Chadema ni utaratibu ambao hautokani na mtu mmoja ama viongozi pekee wa juu bali ni utaratibu shirikishi ambao baada ya kutoka katika hatua ya kura za maoni kitafuata kikao cha kamati ya utendaji ya jimbo kabla ya kamati kuu ya chama kufanya maamuzi yake Februari 14 jijini Dar es Salaam kwa kumteua mgombea atakayesimama jimbo hilo la Kalenga.
Hivyo aliwataka wana Chadema kuwa makini katika kusikiliza kila mgombea na kuhakikisha wanachagua mgombea ambae atakubalika katika chama hicho na hata vyama vingine kikiwemo CCM na wananchi wote wa jimbo la Kalenga.
Kigaila alisema mchakato wa kuchukua fomu ndani ya chama hicho jumla ya wana Chadema 16 walijitokeza kuchukua fomu ila hadi juzi siku ya mwisho kurejesha fomu ni wanachama 13 ndio ambao walirejesha na kudai kuwa mwitikio huo ni ishara nzuri ya Chadema kuonyesha kukua zaidi katika jimbo la Kalenga.
Hata hivyo alisema kuwa Chadema kina imani kubwa ya kushinda kiti hicho cha jimbo la Kalenga na ushindi huo utakuwa ni mwanzo wa kukiondoa chama tawala madarakani .
Kwa upande wake Abwao alisema kuwa CCM kimewasaliti wananchi wa jimbo la Kalenga kwa kuonyesha kuibeba familia ya aliyekuwa mbunge wa jimbo hilo Dr Wiliam Mgimwa na kuwaomba wana Kalenga kuunganisha nguvu zao kumchagua mgombea wa Chadema atakayeteuliwa na Chama .
Awali katibu wa Chadema wilaya ya Iringa vijijini Felix Nyondo aliwataja waliojitokeza kuchukua na kurejesha fomu kuwa ni pamoja na Zubery Mwachura , Dr Evaristo Mtitu, Akbar Sanga, Grace Tendega, Rehema Makoga, Sinkala Mwenda, Henry Kavina, Aidan Pungili, Mussa Mdede, Mchungaji Samweli Nyakunga, Daniel Luvanga, Anicent Sambala na Vitus Lawa.
Hata hivyo wagombea 12 ndio waliofika ukumbini hapo huku mgombea mmoja Zubery Mwachura akikosekana kutokana na kuwa nje ya nchi kwa shughuli za kikazi.
TUSHINDANE KWA AMANI NA UTULIVU MIMI LAIMUSHI
ReplyDelete