February 21, 2014

Hivi ndivyo ilivyokuwa usiku wa Valentine's Day na Skylight Band ndani Thai Village
DSC_0416
Lubea wa Skylight Band alitega mingo lango kuu la kuingilia na kugawa Shots za Tequila pamoja na Sambuka bure kwa wapenzi wa Skylight Band.
DSC_0419
Mashabiki wa Skylight Band wakipata shots za Tequila bure kwenye usiku maalum wa wapendanao uliofana Ijumaa iliyopita ndani ya kiota cha Thai Village Masaki jijini Dar.
DSC_0435
Aneth Kushaba AK47 akiwapa raha mashabiki wa Skylight Band kwenye usiku wa wapendanao juma lililopita huku akisindikizwa na Mary Lucos, Sony Masamba na Sam Mapenzi.
DSC_0611
Wadadaz na Wakaka wakijimwaga na burudani ya Skylight Band.
DSC_0448
Walipendezaje...: Digna Mbepera akifanya yake jukwaani.
DSC_0491
MAJEMBE YA SKYLIGHT BAND....Sam Mapenzi a.k.a asali ya warembo katika hisia kali kwenye nyimbo za malavidavi huku akisindikizwa na Joniko Flower pamoja na Sony Masamba.
DSC_0628
Palikuwa hapatoshi....kama ulikosa juma lililopita basi burudani inaendelea leo pale pale Thai Village.
DSC_0503
Birthday Girl....Meneja wa Skylight Band Aneth Kushaba AK47 (katikati) sambamba na Winfrida Richard pamoja na Digna Mbepera waking'ara kwa jukwaani kwenye usiku wa Valentine's Day juma lililopita.
DSC_0637
Mheshimiwa Bundala anakwambia burudani ya Skylight Band ni Gym tosha, kama anavyoonekana pichani akisebeneka na mrembo.
DSC_0514
Nakupenda pia...Nakupenda Pia...... Collabo ya Ukweeli kati ya Hashim Donode na Winfrida Richard njoo Ijumaa hii usikie kwa masikio yako.
DSC_0525
Surprise.....Ilipotimia saa sita kamili ya kuamkia tarehe 15/2 alizaliwa Meneja wa Skylight Band Aneth Kushaba AK47, waimbaji wenzake waliamua kumuimbia wimbo wa Happy Birthday na kumtakia maisha marefu.....Hujachelewa sana Ijumaa hii unaweza kum-wish belated Happy birthday na kazawadi kidogo....!
DSC_0527
DSC_0529
Champagne zilihusika na kufunguliwa na Mary Lucos pamoja na Sam Mapenzi.
DSC_0531
Mashabiki wa Skylight Band wakimpongeza Aneth Kushaba AK47.
DSC_0538
Kuogeshwa nako kulihusika hajalisha umependezaje...lazima uoge kidogo....! Full Champagne....!!!
Kwa picha zaidi ingia humu

No comments:

Post a Comment

Pages