February 14, 2014

JHIKOMAN AWASHA MOTO SAUTI ZA BUSARA 2014
MWANAMUZIKI nguli wa miondoko ya Afro rege, Jhikoman Manyika   jana usiku Februari 13,  aliwasha moto  kwa kupiga shoo ya nguvu iliyodumu kwa lisaa limoja na kukonga nyoyo umati mkubwa uliojitokeza kwenye tamasha hilo la 11,la Sauti za Busara mwaka huu 2014.

Jhikoman alipanda jukwaani majira ya saa tatu usiku  sambamba na bendi yake ya Afikabisa na kupiga vionjo mbalimbali vya nyimbo zake za sasa na za nyuma.

Jhikoman aliweza kuwasha moto huo kwa kupiga nyimbo zake zilizopo kwenye albamu yake ya Chikonda na nyingine hali iliyokonga wadau hao wa muziki wakiwemo wageni kutoka mataifa mbalimbali na watanzania waliojumukika kwenye tamasha hilo.

Hata hivyo, Jhikoman alisema baada ya shoo hiyo anatarajia kupiga shoo zingine kwenye nchi mbalimbali kwa kufanya ziara maalum ikiwemo mataifa ya Ulaya.

Mbali na Jhikoman wasanii wengine ni pmoja na kundi la Seven Survivor wanopiga muziki wa mchiriku, huku kundi la Baladna taarabu wao walikonga nyoyo kwa muziki wa mwambao na taarabu asili.

Wengine ni kundi la Pongwa kutoka visiwani Zanzibar,  Tritonik (Motius), na nyingine nyingi.

Awali tamasha hilo lilifunguliwa kwa paredi iliyokusanya wanamuziki mbalimbali kutoka mataifa yote na kwa kila mmoja kuonyesha muziki wake mitaani na kasha kumalizikia kwenye viunga vya Ngome Kongwe.

Aidha tamasha hilo la siku nne, linatarajiwa kuwa na wanamuziki mbalimbali vikiwemo vikundi 32, vyenye jumla ya wasanii 200, ambao watapiga shoo kwenye jukwaa hilo la Kimataifa.

Hadi sasa mji wa Zanzibr umebarikiwa kuwa na wageni mbalimbali wakiwemo waliofika maalum kwa ajili ya shoo na wale wanaokuja kupumzika kwenye kisiwa hiki cha marashi ya karafuu.

Aidha, tayari idadi ya wageni imeongezeka  huku baadhi ya hoteli zikiwa zimefurika  na biashara za kitalii zikiwa zinanunuliwa kwa wingi.

Kwa upande wake, David Ojoy ambaye ni msaidizi wa masuala ya habari wa tamasha hilo, anasema kuwa  hali ya wageni imekuwa kubwa kufika kwenye tamasha hilo ikiwemo kupata habari mbali mbali zinazoptikana kwenye mtandao maalum wa tamasha hilo pamoja vyombo vya habari.

"Tunavipongeza vyombo  vya habari kwa kutupa sapoti na tunaomba tuendelee hivyo hivyo ilikukuza muziki wetu wa kiafrika na kujenga tamaduni imara hapa afrika na tamasha hili liendelee kuwa la kimataifa zaidi" alisema Ojay.

No comments:

Post a Comment

Pages