February 14, 2014

KITUO CHA DALADALA CHA BIAFRA CHAGEUZWA SEHEMU YA KUTUPA TAKA
Uchafu ukiwa nyuma ya kituo cha Biafra na ukitizama picha vizuri kuna abiria amekaa lakini cha kusikitisha nyuma yake kuna uchafu ambao unatoa harufu mbaya na pia kuna wafanya biashara katika eneo hili. Sehemu hii imekuwa kero kwa abiria wanaoshuka na hata wanaopanda magari kwenye hiki kituo cha Biafra kilchopo Kinondoni kwani kuna uchafu mwingi unaotupwa na wakazi wa eneo hilo mpaka kituo hiki kubadilishwa na kuwa dampo.
 Hii ndio hali halisi ya kituo cha Biafra kilichopo kwenye wilaya ya Kinondoni jijini Dar es Salaam kilichogeuzwa kama sehemu ya kutupia takataka.
Jambo la kujiuliza ina maana hapa Biafra hakuna Dampo? Au uongozi wa eneo hili umelala mpaka kituo hiki kuwa na hali kama hii inasikitisha sana.  PICHA NA PAMOJA BLOG

No comments:

Post a Comment

Pages