February 04, 2014

Jux: Mimi siringi, ‘bling bling’ ndio maisha yangu


Na Elizabeth John
MSANII wa muziki wa kizazi kipya nchini, Jux, amesema alianza kuvaa nguo za gharama na vidani hata kabla hajawa msanii na yeye kama msanii ni lazima avae hivyo kujitofautisha na watu wengine.

Kauli hiyo ya Jux imekuja baada ya msanii huyo kuambiwa na mashabiki pamoja na wasanii wenzie kwamba analinga kutokana na ‘bling bling’ anazovaa na kwamba muziki anafanya kama kazi yake na sio kuuza sura.

Akizungumza jijini Dar es Salaam hivi karibuni, Jux alisema uvaaji wake umekuwa ukiacha gumzo kwa wapenzi wake pamoja na wasanii wenzie kutokana na kuwa na mvuto zaidi kuliko mastaa ambao wapo juu zaidi yake.

“Mimi ndio nilivyo, hata kabla sijawa msanii nilikuwa hivi, kuongea watu wanaongea sana ukiwa rafu wanasema nipo ‘smart’ wanasema mimi bishoo kwahiyo maneno ya binadamu yapo na mimi napokea kila kitu kutoka kwao maana wao sio mungu,” alisema. 

Aidha, msanii huyo alisema kuwa kamwe hafanyi muziki kama kujifurahisha bali ni kama kazi japo muda mwingi anakuwa masomoni.

“Wengi wanasema mimi ninaringa lakini sipo hivyo hiyo ni kutokana na kutokuzoeana na watu tu, mtu asiyenijua anaweza kusema jamaa anaringa lakini mimi sipo hivyo, unaweza ukanijaji sana lakini nipo kawaida sana,” alisema.

No comments:

Post a Comment

Pages