Na Elizabeth John
MSANII wa filamu za vichekesho nchini, Rashid Mwinshehe ‘Kingwendu’, amesema yupo katika mipango ya kugombea ubunge katika Uchaguzi Mkuu ujao mwaka 2015.
Akizungumza jijini Dar es Salaam hivi karibuni, Kingwendu alisema hawezi kuweka wazi kwa sasa jimbo atakalogombea na chama atakachopitia, kwani bado yupo katika mazungumzo na washauri wake.
“Nimejipanga vya kutosha kuingia bungeni na niko katika mikakati mikubwa, na washauri wangu wa mambo ya siasa wanaendelea kunipika ili niive, lakini habari ndiyo hiyo, naomba Watanzania waniombee tu ili nikawawakilishe,” alisema.
Alisema kwa sasa hataki kuweka wazi chama na jimbo atakalogombea, lakini vuguvugu la uchaguzi likianza tu, ndipo ataweka wazi na kwamba ataingia chama ambacho anaona kinapendwa na wananchi wengi wa jimbo hilo.
Msanii huyo ni kati ya wanaofanya vizuri katika tasnia hiyo, kutokana na umahiri wake katika kazi zake ambazo zinawavutia wapenzi wa filamu nchini.
No comments:
Post a Comment