February 19, 2014

MZEE MAJUTO AFIKIRIA KUKACHA UIGIZAJI


Na Elizabeth John

MCHEKESHAJI mkongwe katika tasnia ya filamu nchini, Amri Athuman ‘Mzee Majuto’, amesema mazingira ya soko la filamu kwa sasa yanamkatisha tamaa na hivyo kumfanya kila wakati afikirie kustaafu na kuhamia katika kilimo.


Mzee Majuto ni kati ya wasanii wanaofanya vizuri katika tasnia hiyo, kutokana na umahiri wake ambao unawavutia wadau wengi wa tasnia hiyo.
Akizungumza jijini Dar es Salaam, Mzee Majuto alisema soko la filamu limekuwa gumu na waliolishikilia wana masharti ambayo kwa msanii unakuwa ni mtihani.
“Yaani mtu unajikuta unaishi maisha ya kubahatisha wakati una kipaji, ni tofauti na ilivyo katika nchi za wenzetu, ningepata mfadhili anipatie trekta, hakika ningeenda shamba na kulima kwa nguvu na kuachana na karaha za kuigiza na kuishi maisha haya ya kubahatisha,” alisema.
Aliongeza kuwa endapo atafanikiwa mpango wake huo, wala hatakuwa na haja ya kuishi mjini, labda mara moja moja tu kwa ajili ya kufuatilia kazi zake za sanaa.

No comments:

Post a Comment

Pages